Klabu ya soka ya Yanga baada yakupata ushindi wa mabao mawili kwa sifuri dhidi ya Namungo katika Dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam wamefanikiwa kuandika rekodi nyingine mpya.
Baada ya ushindi huo sasa Yanga wamecheza michezo tisa na kufanikiwa kushinda yote mfululizo katika Ligi Kuu ya NBC na kuwa timu pekee kufanya hivyo katika Ligi Kuu Bara kwa msimu huu.
Yanga ilianza kupata ushindi Disemba nne mwaka jana dhidi ya Tanzania Prisons kwa bao moja bila wakiwa nyumbani na mpaka jana February nne dhidi ya Namungo wameendeleza wimbi la ushindi.
Katika michezo hiyo tisa Yanga wamefunga mabao kumi na saba na kuruhusu mabao mawili pekee katika mchezo dhidi ya Azam Fc uliomalizika kwa ushindi wa mabao matatu kwa mawili kwao. Yanga walipata matokeo katika michezo ifuatayo;
Yanga 1-0 TZ Prisons
Namungo 0-2 Yanga
Yanga 3-0 Polisi TZ
Yanga 3-0 Coastal Union
Azam Fc 2-3 Yanga
Mtibwa 0-1 Yanga
Yanga 1-0 Ihefu
Yanga 1-0 Ruvu Shooting
Yanga 2-0 Namungo fc
Baada ya mchezo wa Namungo sasa Yanga inaelekea katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika watakaocheza ugenini nchini Tunisia dhidi ya US Monastir.
Yanga na rekodi nyingine ya kibabe katika Ligi
Related Posts
Fadlu Tunaamini anawapa Ubingwa Wekundu
Sambaza…. Kuna usemi usemao ” Simba akikosa nyama hula majani”…..Stori zaidi.
Yanga na Rekodi iliyoshindikana
Mchezo wa soka ni mchezo wa rekodi, pengine ndio mchezo wenye rekodi nyingi kuliko mchezo wowote ule ulimwenguni. Zipo rekodi zilizowekwa, zipo zinazowekwa na kuna ambazo zitakuja kuwekwa katika siku zijazo.