Sambaza....

Mabingwa wa soka Tanzania bara Yanga sc, kesho Jumamosi watakua ugenini kwenye uwanja wa Azam complex kuwakabili wenyeji wao Azam FC

Katika mchezo huo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara, Yanga itawakosa nyota wake saba waliomajeruhi na mmoja akitumikia adhabu ya kuwa na kadi tatu za njano

Wachezaji hao ni Amis Tambwe, Yohana Oscar Nkomola, Abdallah Shaibu, Pato Ngonyani, Pius Buswita Donald Ngoma na Thabani Scara Kamusoko

Taarifa

Tarehe Muda Mwisho
90'

Hafsa habari wa klabu hiyo Dismas Ten, tayari ameweka wazi kuwa watawakosa nyota hao saba katika mchezo huo wa kesho

“Tutawakisa wachezaji wetu saba katika mchezo wetu wa kesho dhidi ya Azam FC, lakini wengine wapo tayari na mchezo huo ambao tutalazimika kushinda ili kujiweka vizuri kwenye msimamo wa ligi

Aidha pia klabu hiyo itamkosa kocha wake msaidizi Shadrack Nsajigwa, anayesafiri kwenda kwenye msiba wa shemeji yake, huku kibali cha kufanyia kazi cha kocha mkuu George Lwandamini ikiwa ni kitendawili

Endapo kitakosekana kibali hicho, ina maana Yanga kesho itaongozwa na mwalim wake wa viungo Noel Mwandila raia wa Zambia

PosTimuPWDLFAGDPts
1Simba SC2091444718413124289479
2Yanga SC2001374320334117217454
3Azam FC2051135339307150157392
4Tanzania Prisons202587668174193-19250
5Kagera Sugar FC205606976171212-41249
6Coastal Union FC173565562141167-26223
7Mtibwa Sugar FC195565584178220-42223
8KMC FC173525764165185-20213
9Mbeya City FC166455764153185-32192
10Namungo FC13649444315013911191
11Ruvu Shooting166455071146200-54185
12JKT Tanzania SC11332473487100-13143
13Mwadui FC108333243119134-15131
14Lipuli FC10733324298116-18131
15Biashara FC1062839398297-15123
16Mbao FC10730324586120-34122

Sambaza....