Leicester City vs Everton
TIMU ZOTE KUFUNGANA.
Kwanini ?
Mechi tano zilizopita za timu zote ni mechi moja tu ambayo timu zote hazijafanikiwa kufunga goli. Hii inaonesha safu zao za ushambuliaji siyo butu.
Na katika hizo mechi tano zilizopita Leicester City imefanikiwa kupata cleansheets 2 tu na kufungwa magoli 7.
Huku Everton wakifanikiwa kupata clean sheet moja tu katika mechi tano zilizopita huku wakifungwa magoli 7.
Tottenham Hotspurs vs Cardiff City.
SPURS KUSHINDA.
Kwanini ???
Hii ni mechi ya tatu kukutana kwa hizi timu kwenye ligi kuu na Tottenham Hotspurs wakashinda mechi zote tatu kwa goli 1-0 tangu mwaka 2012.
Cardiff hawajawahi kushinda mechi yoyote kwenye mashindano yote kwenye mechi saba ambazo wamecheza dhidi ya spurs tangu January 1978.
Kwenye mechi saba ambazo spurs kacheza na Cardiff kwenye uwanja wake wa nyumbani, spurs ameshinda zote na kufunga magoli 19.
Tottenham hawajawahi kufungwa na timu yoyote iliyopanda daraja katika mechi 37
Katika mechi 15 walizocheza nyumbani wameshinda mechi 13.
Leeds vs Brentford
Timu zote kufungana.
Middlesbrough vs Nottingham forest
MIDDLESBROUGH KUSHINDA AU KUTOKA SARE.
Mechi tano Middlesbrough imeshinda mechi 2 na kudraw mechi 3. Nottingham forest imeshinda mechi tatu na kudraw mbili.
Bayern Munich vs Borrusia M’Gladback
TIMU ZOTE KUFUNGANA.
Tangu ligi ianze Borrusia M’Gladback imefunga goli kwenye kila mechi na kufunga magoli 12 huku ikifungwa magoli 7. Huku Bayern Munich wakiacha kufunga dhidi ya Hertha Berlin walipofungwa 2-0. Mpaka sasa wamefunga magoli 12 na kufungwa magoli 5