Kila baada ya msimu wa mashindano kukamilika shirikisho la mpira wa miguu la Tanzania(TFF) limekuwa na utaratibu wa ugawaji wa tuzo kwa washindi katika vipengele mbalimbali.
Kama zilivyo taasisi nyingi huongozwa kwa kanuni na katiba maalumu ambayo maamuzi na uendeshaji wa taaaisi hizo huegamia, basi la shirikisho(TFF) huongozwa nazo.
Msimu wa ligi kuu ya NBC 2022/23 umemalizika na umetamatika rasmi na hafla za ugawaji tuzo uliofanyika pale Tanga juni 12. Kulikuwa na maswali mengi juu ugawaji wa tuzo hizo kutokana na baadhi ya vipengele kuwa na mshindi zaidi ya mmoja, kumekua na uzushi kwamba pengine hakuna kanuni zinazoeleza wazi mshindi anapatikanaje, mfano ligi kiliyomalizika kipengele cha mfungaji bora wa ligi ilikuwa na washindi wawili Fiston Mayele na Saido Ntibazonkiza baada ya wote kufunga goli 17 kila mmoja.
TFF haijaweka kanuni ambazo zitaamua mshindi endapo kipengele kitakuwa na washindana wanaofanana kitakwimu na hii imekua tatizo kiasi kwamba inaleta mgawanyo na mpasuko miongoni wa wadau wa soka, licha ya mkanganyiko huo lakini wadau wengi wa soka hawana utaratibu wa kusoma na kuzijua kanuni pengine kuna baadhi ya mambo yako kikanuni na yanatambulika badala yake wanabaki kulaumu na kuzua taharuki.
Kila ligi duniani huwa na kanuni zake za uendeshaji na hizo huwa ndo hakimu wa mambo yote, ligi ya Tanzania nayo huongozwa kwa kanuni na sheria mahususi, hivyo ili kuepuka baadhi ya maswali na mpasuko kwa baadhi ya wapendakandanda basi msimu mpya wa mashindano unapoanza shirikisho litangaze kanuni zitakazotumika katika uongozaji wa ligi pamoja na vipengele vya washindi wa tuzo na miongozo ya upatikanaji washindi.
Lakini vipi kuhusu tuzo ya mchezaji bora wa mechi?
Ligi ya Tanzania (NBC) ipo na utaratibu wa kutoa tuzo kwa kocha na mchezaji bora wa mwezi, lakini limekuwa swali gumu juu ya mchezaji bora wa mechi hakuna tuzo kwa ajili ya wachezaji bora wa mechi. Kwani kanuni juu ya mchezaji bora wa mechi hazipo? Na kama zipo je zinatekelezwa ipasavyo?
Tuzo ni kipengele nyeti sana pengine naweza kusema huweza kuwa kivutio cha wachezaji wengi wakubwa toka mataifa mengine lakini tuzo zinaweza kuchagiza muamko wa wachezaji wa ndani, ushauri wangu kwa bodi ya ligi na shirikisho kuhakikisha tuzo zinapata mvuto zaidi;
• Kutafuta wadhamini wa kudhamini tuzo, pengine tuna walaumu bodi ya ligi na shirikisho lakini sababu kuu ni kutokuwepo kwa wadhamini wa kudhamini tuzo hizi, mataifa yaliyoendelea hususani mataifa ya Ulaya huweka zabuni ili kupata wadhamini wa tuzo zao mfano pale england wapo Backlays wanadhamini wa tuzo za ligi hiyo, makocha na wachezaji bora wa mwezi pamoja na wachezaji bora wa mechi.
Hivyo bodi ya ligi na shirikisho watangaze dhabuni ili tupate wadhamini wa tuzo katika ligi yetu
•Kanuni juu utolewaji tuzo na vigezo vyake viwekwe wazi kabla ya msimu wa mashindano kuanza, hii itasaidia kuepuka baadhi ya migongano ya kimaamuzi pale washindi wanapofanana vigezo vya kupokea tuzo na hii itaongeza mvuto zaidi na pia itawarahishia wadhamini katika masuala mazima ya uandaaji wa tuzo hizo.
NB: SIZONJE