Sambaza....

Tumekukusanyia mambo 10 ambayo kocha mkuu wa klabu ya Yanga ameyazungumza kwa masikitiko sana. Tupe maoni yako pia katika sehemu ya maoni.

1: Jana ilikuwa dirisha dogo la usajili linafungwa ni siku ambayo uongozi wa Yanga umefanya vitu vya ovyo sana.

2: Nilifikiria kuwaachia timu yao , ila nikambuka jinsi wanachama wanavyoipenda timu yao nikaamua kubaki.

3:Sipo Yanga kwa ajili ya pesa, nipo kwa ajili ya kuipambania timu hii kutokana na mashabiki wanavoipenda timu na ushirikiano wanaonipa.

4:Siku ya Alhamisi niliambiwa wamewasainisha tayari Mshambuliaji wa Uganda, kipa wa Kenya na winga wa Mwadui. Niliwapongeza kwa hilo.

5:Jana usiku saa 5, napigiwa simu na mshambuliaji Mganda kuwa amesaini Egypt nikawauliza viongozi wa Yanga wakanijibu wamefanikiwa mchezaji mmoja tu ambaye ni Haruna Bobani.

6:Tulikubaliana kuwa mzunguko wa kwanza tusifanye usajili mkubwa, ila dirisha dogo tusajili walinipa masharti kuwa niwe nafasi ya pili au tatu.

7:Kwa mambo haya wanayofanya, nisiulizwe kuhusu ubingwa wala nikipoteza mchezo dhidi ya Simba maana viongozi ni wababaishaji.

Reuben Bomba

8:Reuben Bomba ni Mreno pia ana uraia wa Congo ni mchezaji mzuri sana, na tulikubaliana apewe mkataba wa miezi sita, kwa kuwa alikuwa anaenda ulaya na alikuwa anasubiria viza yake, lakini nashangaa kwenye mitandao viongozi wanadai mimi ndo nimemkataa. . ntamkataa vipi mchezaji mzuri kama yule.

9:Timu haina hela wachezaji wana matatizo mengi na hawajui lini watalipwa lakini wanacheza kwa moyo wote, angalia Makambo hajalipwa hata sent ya usajili na juzi hapa mizigo yake ilizuiliwa hotelini kwa kuwa hajalipa gharama za chumba.

https://www.instagram.com/p/BrcPygtg4_i/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=lrg4gdhknifj

10:Niliwaambia waniletee kipa wa Kenya, wanasajili kipa hata simfahamu na wala sikumpendekeza hata sijui anaitwa nani na anatoka wapi hii ndo huwa naita kitu ya ovyo.

Nini maoni yako?

Sambaza....