Inawezekana siku za hivi karibuni ligi kuu ya Tanzania bara itarudi tena baada ya kusimama kwa muda mrefu. Matumaini hayo yamekuja mara baada ya raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli kutoa matumaini hayo.
John Kombe Magufuli amedai kuwa kama hali itaendelea kuwa vizuri anafikiria namna ya kufungua vyuo na shughuli mbalimbali za michezo ambazo zinaonekana ni sehemu za burudani kwa wananchi.
Kauli hii ni ya matumaini , wengi tunasubiri ligi ianze . Wakati tunasubiri ligi kuanza kuna taarifa mbalimbali za usajili zinazoendelea katika timu mbalimbali hapa nchini.
Kuna taarifa ya Yanga kumwihitaji kiungo wa klabu ya Rayon Sports ya Yanga , Kakule Fabrice. Kiungo huyo amedai kuwa ashawahi kuongea na viongozi wa Yanga hivo anasubiri majibu.
“Niliwahi kutafutwa na kiongozi ambaye alijitambulisha kuwa ametoka GSM , niliongea naye akaniomba nimtumie video zangu na Mimi nikafanya hivo , kwa hiyo mpaka sasa hivi nasubiri majibu kutoka kwao” – alidai kiungo huyo fundi ambaye wengi wanadai ni hatari kuzidi Chama wa Simba.
Alipoulizwa kuhusu mkataba wake na Rayon Sports , Kakule Fabrice amedai kuwa mkataba wake na Rayon Sports umebaki mwezi mmoja kwa hiyo mpaka sasa hivi wako kwenye mazungumzo.
“Nimebakiza mwezi mmoja kwenye mkataba wangu na Rayon Sports. Tuko tunajadiliana kuhusu mkataba mpya , ikishindikana nitaona wapi nitaenda iwe Kenya au Tanzania”- alidai kiungo huyo anayeweza kucheza namba 6 na namba 8 kwenye uwanja.