Uongozi wa klabu ya Yanga umekiri kupokea barua nyingine kutoka kwa golikipa namba moja wa timu hiyo Beno Kakolanya ya kutaka kuvunja mkataba wake licha ya kulipwa stahiki zake alizokua akiidai klabu hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo kariakoo jijini Dar es salaam, Kaimu mwenyekiti wa Yanga Samwel Lukumay amekiri kuwa wamepokea barua kutoka kwa golikipa wao huyo akitaka kuvunja mkataba wake, hivyo wao kama uongozi watakaa na kulitolea ufafanuzi suala hilo kulingna na kanuni za mkataba huo.
Wakati huohuo Lukumay amewaomba wapenzi wa Yanga kuacha kumpigia simu na kumtisha kocha Mwinyi Zahera na badala yake kumuunga mkono kwani kila anachofanya kina baraka za uongozi wa Klabu.