Klabu ya Yanga imeendelea na uhamasishaji wa mashabiki ili wajitokeze kwa wingi kuelekea mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe. Katika kuhakikisha uwanja wa Mkapa unajaa siku hiyo matawi ya wilaya ya Temeke walikua na shughuli ya uhamasishaji iliyofanyika Mbagala Zhakiem na kuhudhuliwa na viongozi watendaji mbalimbali wa klabu ya Yanga.
Katika zoezi hilo alikuepo Afisa habari wa klabu ya Yanga Ali Kamwe ambae hakusita kuwaita Wananchi siku ya Jumapili ili kuwashangilia wachezaji wao na kuiteketeza TP Mazembe.
“Tujae pale Kwa Mkapa rangi ziwe tatu tuu kijani, njano na nyeusi halafu tushangilie kwanguvu tuone kama TP Mazembe watatoka. Simba watanikumbusha, ule uwanja wao kule Congo unaingiza watu 17,000 tu hivyo Mazembe hawajawahi kucheza katika uwanja wenye ukubwa kama huu na mashabiki wengi hivyo,” alisema Ali Kamwe afisa habari wa klabu ya Yanga.
Nae mshambuliaji kinara na kiongozi wa Yanga Fiston Mayele amewahakikishia mashabiki, wapenzi na wanachama wa Yanga Jumapili atakua Mayele watofauti kabisa na yupo tayari kuiongoza Yanga kuiteketezaTPMazembe.
“Nawahakikishia Jumapili mtamuona Fiston Kalala Mayele wa tofauti. Mtamuona Mayele wa tofauti zaidi ya ile ya Zaalan na wa mechi ya Ngao ya Jamii (dhidi ya Simba),” alisema Fiston Mayele.