Sambaza....

Kikosi cha Yanga kitashuka dimbani leo saa moja jioni katika mchezo wa Kundi D wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa nchini Mali katika dimba la Stade 26 Mars dhidi ya Real Bamako.

Mpaka sasa Yanga wana alama tatu walizozipata katika michezo miwili baada ya kufungwa moja ugenini dhidi ya US Monastir na kushinda mchezo mmoja nyumbani dhidi ya TP Mazembe na hivyo kuwafanya Wananchi kushika nafasi ya pili.

 

Baada ya ushindi wa mabao matatu kwa moja dhidi ya TP Mazembe umewafanya Yanga kuwa na hesabu nzuri zakufuzu hatua inayofuata huku ushindi ama sare katika mchezo wa leo utazidi kuwaweka Yanga katika nafai nzuri kwenye kundi lao.

Kinara wa kundi hilo US Monastir mwenye alama nne atakua ugenini kucheza dhidi ya TP Mazembe wenye alama tatu baada yakupoteza mchezo wa mwisho mbele ya Yanga na hivyo kupelekea mchezo mwingine mgumu katika kundi D.

Kwa hesabu zozote zile leo Yanga hawapaswi kupoteza mchezo  kama itashindikana alama tatu basi angalau wapate alama moja ili kuendelea kuweka hai matumaini yao ya kufuzu robo fainali katika michuano hiyo yapili kwa ukubwa Afrika katika ngazi za vilabu.

Sambaza....