Mchezo wa soka ni mchezo wa rekodi, pengine ndio mchezo wenye rekodi nyingi kuliko mchezo wowote ule ulimwenguni. Zipo rekodi zilizowekwa, zipo zinazowekwa na kuna ambazo zitakuja kuwekwa katika siku zijazo.
Zipo rekodi zilizowekwa zikavunjwa na zipo rekodi zilizowekwa zimeshindikana kuvunjwa. Kila uchwao zinawekwa rekodi ila zipo rekodi ambazo zinabaki kuwa ndoto ngumu kuzifikia lakini inawezekana. Wapo wachezaji na vilabu vya soka duniani vimeweka rekodi za kipekee sana ambazo haikuwa rahisi kuziweka na itachukua muda kuvunjika …. wapo Real madrid na rekodi yao ya vikombe vingi ligi ya mabingwa (15), Leonel messi na tuzo zake za ballon d’or(8) , Cristiano Ronaldo na rekodi zake za magoli mengi zaidi kwa wachezaji wanaocheza (900+) na rekodi nyingine kibao.
Mchezo huu una rekodi nyingi za kustaabisha ila wanachotaka kukifanya/ kukiweka YANGA kitakustaajabisha. Katika msimu huu wa ligi kuu NBC Tanzania Yanga wamecheza jumla ya michezo minane na kujikusanyia alama 24 zaidi kuliko timu yoyote msimu huu ikiwa na wastani wa asilimia 100% za ushisndi. Mkubwa zaidi kuliko timu yoyote katika ligi ya NBC msimu huu na hawajaruhusu bao mpaka sasa.
Baada ya kushinda na kuwa mabingwa kwa misimu mitatu mfululizo, Yanga msismu huu wanataka kuwa mabingwa kwa mara ya nne mfululizo na kuweka rekodi ya kushinda michezo yote ya ligi bila kupoteza wala kuruhusu bao.
Je itawezekana?
NDIO, inawezekana japo ni ngumu sana. yapo maoni na malalamiko kutoka kwa wadau wa soka kuwa Yanga inashinda ila haichezi vizuri kama msimu uliopita. Lakini wanatakiwa kufahamu kuwa Miguel Gamondi kocha wa Yanga ameibadilisha yanga kutoka kumiliki mpira mda wote wa mchezo badala yake anaifanya timu yake iwe hatari katika vipindi vyote vya mchezo hususani vipindi vya mpito. Safu ya ulinzi ya yanga imekuwa imara sana msimu huu, hii inatoa ishara kwamba ni wagumu sana kufungika kwani hawajaruhusu bao na wastani wa makosa wanayofanya kupelekea wao kufungwa ni mdogo mno.
Taarifa
Tarehe | Muda | Ligi | Msimu | Mwisho |
---|---|---|---|---|
02/11/2024 | 4:00 pm | TPL | 2024-2025 | 90' |
Katika michezo yao nane mpaka sasa katika NBC premier league safu yao ya ulinzi imekuwa ngome ngumu sana kwa washambuliaj wa timu pinzani. Wamekutana na kagera sugar ugenini pale kaitaba bukoba wakashinda mbili sifuri, kisha ugenini dhidi ya kengold pale sokoine mbeya wakashinda moja bila kisha dhidi ya KMC pale chamazi wakashinda goli moja bila, kisha dhidi ya pamba fc pale chamazi complex yanga wakapata ushindi mnono wa goli nne kwa bila. Oktoba 19 wakakutana na simba sc wakaigalagaza simba goli moja kwa bila, kisha wakashinda mbili bila dhidi ya JKT pale chamazi, dhidi ya coastal union pale sheikh Amri Abeid Arusha yanga wakashinda moja bila, halafu wakasafiri mpaka visiwa vya marashi Zanzibar na kumenyana na Singida black stars ndani ya New Amani Complex (30/10/2024) na kuibuka na ushindi wa goli moja kwa bila.
NB: Mechi ijayo Yanga wanakuwa wageni wa waoka mikate wa chamazi (AZAM) katika dimba lao CHAMAZI COMPLEX. je Yanga wataweza kuendeleza rekodi yao ya kushinda bila kuruhusu bao?
Basi usihofu KANDANDA .CO.TZ inakundalia majibu na taswira kuelekea mchezo huo. Endelea kubaki nasi na karibu katika ULIMWENGU WA KANDANDA.