Sambaza....

Kocha mkuu wa Yanga sc, George Lwandamina amepanga kuutumia mchezo wa kesho dhidi ya Singida United kuwa sehemu maandalizi ya kikosi chake kuelekea katika mchezo wa marejeano na Wolaita ditcha Jumanne ijayo Aprili 17, 2018

Yanga inataraji kuvaana na Singida United kesho, kunako uwanja wa taifa jijini Dar es salaam katika muendelezo wa michezo ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.

TareheMwenyeji-Mgeni

Akizungumzia mchezo huo, Lwandamina alisema mchezo dhidi ya Singida utakuwa mgumu lakini wamejipanga kushinda ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutetea ubingwa wao

“Singida United ni timu nzuri na tumetoka kucheza nao wiki iliyopita kila mtu ameona matokeo, maana yake mchezo wa kesho utakuwa mgumu na hata wachezaji wangu wanalijua hilo, pia tutatumia mchezo huo kama maandalizi yetu ya mechi ya marejeano na Ditcha”

Singida United waliiondosha Yanga sc, kunako michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) hatua ya robo fainali kwa penati 4-2 kufuatia sare ya 1-1 ndani dakika 90, za kawaida kunako uwanja wa Namfua mjini Singida

Sambaza....