Sambaza....

Wananchi Yanga wanatarajia kucheza mchezo wao wakwanza ugenini dhidi ya El Merreck ya nchini Sudan lakini mchezo huo unatarajiwa kuchezwa nchini Rwanda kutokana na machafuko ya nchini Sudan.

Kuelekea mchezo huo wa raundi ya kwanza wa Ligi ya mabingwa Afrika ugenini wametangaza utaratibu kwa mashabiki wanaotaka kwenda kuisapoti Yanga nchini Rwanda.

 

Akiongea na Wanahabari  msemaji wa klabu ya Yanga amesema ” Tutakwenda Kigali Rwanda na mashabiki wetu, Tutaondoka na mabasi kuelekea nchini Rwanda kwa gharama ya 150,000 tu, hii itahusika kwenye usafiri pekee,” alisema na kuongeza;

“Gharama za kula na kulala itakua ni juu yenu mashabiki, pia kila anaesafiri anapaswa kuwa na hati ya kusafiria maana tunaenda nje ya nchi wala sio Mbeya.”

Kuelekea safari hiyo Kamwe amewaita mashabiki na kuwataka kuungana nao ili kwenda kuweka historia mpya nchini Kigali Rwanda.

Mashabiki wa Wananchi Yanga.

“Tunakwenda Rwanda tarehe 14 na kule tunakwenda kuweka historia si tu ndani ya uwanja lakini pia mpaka nje ya uwanja pia. Twendeni pale Kigali tukaweke historia kama Yanga.

Tayari mabasi manne yameshajaa kutoka mikoani, mawili tayari pale Kakonko wameniambia mabasi mawili yamejaa, Mwanza basi moja limejaa na Kagera hata kabla ya sisi kutangaza leo hii safari,” alimalizia Kamwe.

Sambaza....