Kama ilivyo ada mchezo wa Watani wa Jadi huchezwa siku moja lakini matokeo yake hubaki ama huishi muda mrefu zaidi kutokana na ukweli kwamba matokeo ya mechi hiyu huishi muda mrefu.
Kocha Robert Oliveira “Robertinho” tangu atue nchini katikati ya msimu uliopita hakuwahi kupoteza mchezo hata mmoja wa Ligi lakini kipigo cha mabao matano kutoka kwa Mtani kimemfanya kupoteza kibarua chake, hivyo kufuzwa kwa kupoteza kwa mechi moja pekee ya Ligi.
Kupitia taarifa rasmi ya klabu kwa umma Simba ilisema “Klabu imefikia makubaliano ya pande zote mbili kuvunja mkataba wa kocha mkuu wa kikosi cha kwanza Rovert Oliveira (Robertinho).”
Si tu Robertinho lakini pia kocha wa viungo wa klabu hiyo Corneille Hategimana pia amekwenda na maji. Hategikana huyu aliletwa nchini na Robertinho kwani waliwahi kufanya kazi pamoja nchini Rwanda.
Kikosi cha Simba sasa kitakua chini ya Daniel Cadena na Selemani Matola ambao watakua makocha wa mpito huku mchakato wa kutafuta kocha mpya ukiwa tayari umeshaanza rasmi.
Pasi na shaka kipigo cha mabao matano kutoka kwa Yanga kilikua kikubwa kwa Simba na hivyo kuwafanya viongozi kuchukua hatua yakulipunguza benchi la ufundi na kuanza upya katika kusaka kocha mkuu.