Sambaza....

Baada ya jana mkuu wa kitengo cha habari cha Azam FC , Zaka za Zakazi kuwatuhumu Yanga kuandika barua wakijifanya ni Salum Abubakary “SureBoy” leo hii Afisa habari wa Yanga , Hassan Bumbuli amedai kuwa wao hawamtaki Salum Abubakary “SureBoy”.

Hassan Bumbuli amedai kuwa ni kweli walipeleka barua Azam FC ya kumtaka kumsajili Salum Abubakary “SureBoy” lakini baada ya kutojibiwa wameamua kukaa kimya na hawamtaki kwa sasa mchezaji huyo.

“Ni kweli tulipeleka barua ya kumtaka Salum Abubakary “SureBoy” kiweledi kabisa Azam FC wakatujibu kwa kutuomba tuandika ofa tuliyonayo na sisi tukaandika milioni 20″.

“Baada ya kuandika milioni 20 Azam FC walisema ni ndogo walitutaka tuje na milioni 70, sisi tukaandika barua ya pili yenye ofa ya milioni 35 ambayo mpaka sasa hivi haijajibiwa na sisi tumeamua kuachana na mchezaji tunafuata mchezaji mwingine”- alimalizia Hassan Bumbuli.

Salum Abubakary “SureBoy” amebaki kama mchezaji pekee wa Azam FC ambaye alipambana kuipandisha timu ya Azam FC daraja kutoka ligi daraja la kwanza mpaka ligi kuu.

Ndiye mchezaji mwandamizi kwa sasa kwenye kikosi cha Azam FC baada ya wenzake kama kina John Bocco kuondoka. Baba yake Salum Abubakary “SureBoy” aliwahi kuichezea Yanga pia siku za nyuma

Sambaza....