Sambaza....

Tangu mwaka  1966, TP Mazembe imekujikusanyia jumla ya mataji 24 kwa ngazi ya taifa na 11 kwa ngazi ya  kimataifa. Ndio klabu yenye mafanikio makubwa  zaidi nchini ikiwa na jumla ya mataji 35.

Ligi kuu.

Katika ligi yao, inayofahamika kwa jina la Linafoot, Mazembe wamebeba mara 16, yaani mwaka 1966, 67, 69, 76, 87,2000,2001, 2006, 2007, 2009, 2011, 2013,2014, 2016 na 2017. Na hii ni rekodi ambayo haijavunjwa.

Shirikisho (Coupe du Congo)

Mashindano haya, kwa Tanzania unaweza kuyafananisha na Azam Sports Federation Cup. Kwa upande wa Congo, yanafahamika kwa jina la Coupe Du Congo.

TP imebeba mara  5 mwaka 1966,67, 76, 79, na 2000  .  Klabu ya DC Motema Pembe ndio klabu yenye mafanikio makubwa na kombe hili ikibeba mara 12.

DR Congo Super Cup (Ngao ya Jamii)

Hii ni mechi inayochezwa kati ya mshindi wa ligi , Linafoot na mshindi wa kombe la shirikisho, Coupe du Congo. TP Mazembe imebeba mara  3 yaani mwaka 2013, 2014, na 2016. Hii ni rekodi ambayo haijawahi fikiwa na klabu yoyote nchini Congo.

Kwa Afrika:

Klabu Bingwa Afrika. TP Mzembe imebeba mara 5 kombe la hili. Mwaka 1967, 68, 2009, 2010, na  2015. Ilibatika kuingia fainali mara mbili bila kuchukua na kuishia nafasi ya pili, hii ilikuwa ni mwaka 1970 na 1971.

Shirikisho Afrika.

Taji hili wamefanikiwa kulichukua mara 2  mfululizo mwaka 2016 na 2017. Mwaka 2013 waliingia fainali na kupoteza  mbele ya  Club Sportif Sfaxien ya Tunisia.

Wajue TP Mazembe, rekodi na wachezaji wao..

CAF Super Cup.

Hili ni kombe linalohusisha timu  mbili, moja ilishinda kombe la shirikisho na ile iliyoshinda kombe la klabu bingwa Afrika kwa mwaka huo. TP Mazembe imefanikiwa kuchukua kombe hili mara  3, mwaka 2010, 2011 na 2016,  na ikidunguliwa mara mbili yaani 2017 na 2018.

Na mafanikio makubwa kabisa kwa TP Mazembe  katika uwanda wa kimataifa ( duniani) ni kutinga fainali  ya mashindano ya klabu bingwa ya dunia mwaka 2010.

TP Mazembe ilitinga fainali za mashindano hayo maarufu duniani na kisha kufungwa na timu ya Internazionale  ya nchini  Italia.


Sambaza....