Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Manchester United, Wayne Rooney, aliecheza kwa mfanikio katika klabu hiyo kabla ya kurudi tena katika klabu yake ya awali ya Everton FC, anatarajia kwenda marekani. Imeripotiwa na skysports.com kuwa kwa sasa yupo katika mazungumzo na klabu ya DC United yenye makazi yake pale Washington DC.
Vyanzo vinasema, Rooney huenda pia akafanya vipimo vya afya pia kujiunga na timu hii iliyo MLS.
Miaka | Timu | Mechi | Magoli |
2002–2004 | Everton | 67 | 15 |
2004–2017 | Manchester United | 393 | 183 |
2017– | Everton | 31 | 10 |
-Rekodi za Wayne Rooney.
Habari nyingine za Uhamisho:
Fred kuelekea Manchester United
Mazungumzo yanaendelea vizuri kati ya Manchester United na kiungo Mbrazili wa Shakhtar Donetsk, Fred, mwenye miaka 25. Man Utd wanakimbizana na muda kabla ya kuanza kwa kombe la dunia huko Urusi.