Vijana wawili wa Kitanzania ambao ni miongoni mwa wachezaji kumi waliochaguliwa kujiunga na Vituo vya Soka kutoka Ulaya. Vijana hao wanaungana na wenzao kutoka katika mataifa tofauti, walipatikana kupitia Showcase ya sika kwa vijana chini ya miaka 20 ilivyofanyika kwa takribani wiki moja nchini Nigeria.
Katika tukio hilo kulikuwa na na maskauti wa mataifa mbalimbali. Showcase hiyo ilihusisha wachezaji sabini kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika na jumla ya vijana 10 walichaguliwa wakiwemo Watanzania wawili ni Aboubakar Mligite na Mohammed Fundi.
Msafara huo uliongozwa na Kocha mbobezi wa soka la Vijana Juma Maswanywa ambaye hufanya kazi kwa ukaribu na mdau wa mtandao huu wa Kandanda.co.tz, Tigana Lukinja.
Mataifa yaliotoa wachezaji hao kumi ni Nigeria (5), Ivory coast (3) na Tanzania (2).
Hivi karibu katibu mkuu wa Shirikisho la Soka la Tanzania, TFF, Ndugu Kidao, alinukuliwa akisema kuna wachezaji Watanzania zaidi ya 21 wanacheza nje ya nchi, shirikisho linafuatilia kwa ukaribu. Milango hii kwa Mligite na Fundi inaendelea kufunguka zaidi kwa kuongeza wachezaji Watanzania ambao wanaweza kuibuka katika vituo vya Soka.