Sambaza....

Jana Yanga ilicheza na Namungo FC katika mechi za.mwendelezo wa ligi kuu Tanzania bara kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Yanga alitoka sare ya magoli 2-2.

Magoli ya Namungo FC yalifungwa na Manyama ambaye alifunga magoli yote mawili huku magoli ya Yanga yalifungwa na David Molinga ambaye alifunga magoli yote mawili.

David Molinga “Falcao”

Baada ya mchezo huo kocha mkuu wa Yanga , Luc Eyamel alisema kuwa timu imecheza vizuri ila tatizo ni washambuliaji ambao ni butu .

“Nafikiri mmeona timu ilivyocheza, ilitakiwa kipindi cha kwanza tupate magoli hata matatu lakini hakuna goli tumefunga. Hawa washambuliaji wetu butu Sana mnataka Mimi niingie nifunge? Nafasi zinatengenezwa lakini umaliziaji mbovu” – Alisema Luc Eyamael.

Alipoulizwa kuhusu kumwingiza Abdullaziz Makame ambaye ni kiungo mkabaji ambaye aliingia kuchukua nafasi ya mshambuliaji , Luc Eymael alidai kuwa yeye alikuwa anajua anachokifanya.

Makame

“Nimemtoa mshambuliaji nikamwingiza kiungo mkabaji ambae ametoa pasi ya goli, mlifikiri Mimi ni mjinga? Mimi nafikiri vizuri zaidi yenu ndio maana tumerudisha magoli mawili.” Alisema kocha huyo kutoka Ubelgiji

Alipoulizwa kuhusu viwango vya waamuzi kwenye mchezo huo ,kocha huyo alidai kuwa waamuzi wanachezesha katika kiwango ambacho yeye hafurahishwi nacho kwa kiasi kikubwa.

“Zaidi sifurahishwi na mazingira ya marefa, beki wangu anapiga shuti lina mgonga beki wa timu pinzani refa anasema offside! inawezekana vipi ?” Alimalizia kocha huyo ambaye yeye na timu yake ya Yanga wamepata sare tatu mfululizo dhidi ya JKT Tanzania,  Azam FC na Namungo FC

Sambaza....