Sambaza....

Mlipuko wa corona umeathiri kwa kiasi kikubwa shughuli nyingi za kijamii lakini pia katika sekta ya michezo pia imeguswa na haswa katika mpira wa miguu. Barani Ulaya Ligi na michuano mbalimbali imesimamishwa ili kuepusha kuenea zaidi kwa ugonjwa huo.

Tamko la TFF la kusimamisha Ligi Kuu, Ligi daraja la kwanza, Ligi daraja la pili na michuano mingine mbalimbali kwa wadau na wanachama wake limepokelewa tofauti na wadau mbalimbali na wachezaji wenyewe pia.

Baki salama nyumbani zingatia maagizo ya wataalamu wa Afya.

Tovuti ya Kandanda inakuletea maoni ya baadhi ya wachezaji wa Ligi Kuu na daraja la kwanza.

David Uromi  wa Alliance Fc “Sioni kama kusimama kwa Ligi  kuna athari sana maana afya ni bora kuliko kucheza. Lazima tukubaliane na mazingira kwa sasa hali hairuhusu tusubiri tamko la Serikali hadi litakaporuhusu. Kwa timu gharama za uendeshaji zinakuwa kubwa kwasababu wanakuwa tayari na bajeti yao ya msimu mzima.”

John Mbisse kiungo wa Namungo fc.

John Mbise kiungo wa Namungo fc “Kujilinda kama ilivyoelezwa na wataalam wa afya kwamba tukwepe mikusanyiko iliyozaidi ya watu kumi. Lakini kama Mtanzania kama unavyojua maisha yetu ni ya kimaskini lazima utoke nje ndo upate chochote kitu ivyo tutajitahidi kujilinda ili kukwepa ugonjwa wa corona”

James Msuva wa KMC “Kwa team tulikuwa na muendelezo mzuri but tunapata mda wakujiandaa zaidi,,,,kwangu kawaida tu tatizo hofu kwa familia na nchi kwa ujumla.”

Kevin Kongwe Sabato “Kevi Kiduku”

Kevin Sabato Kagera Sugar “Ligi ilikua inaenda vizuri lakini kwa bahati mbaya imetokea corona na kusimamisha ligi, kwa kiasi fulani inatupunguza kasi.”

Adam Balle Ruvu Shooting “Kwakiasi fulani huu ugonjwa umetuathiri kama wachezaji na timu pia. Lakini kwa kuzingatia afya na uhai wa  wachezaji pia na mashabiki ni sahihi kwa Ligi kusimama.”

Sambaza....