Sambaza....

Kama nawasikia ndugu zagu Wadigo na Wasambaa pamoja na Wazigua katika barabara zote za mitaa pale Tanga wakiuliza hili swali.
Jioni ya leo majira ya saa 10:00 jioni pale Mkwakwani patakuwa hapatoshi kwenye mechi kati ya wenyeji Coastal Union ‘wanamagushi’ .

YouTube player

Natambua mchezo hautakuwa mwepesi kwa pande zote mbili wenyeji na wageni wao ‘Wanalunyasi’. Kwanini basi utakuwa na ushindani mkubwa hivyo? Binafsi nawaangalia kwenye nafasi walizonazo sasa.

Simba ipo nafasi ya pili akiwa kwenye mbio za ubingwa dhidi ya watani wao Yanga ambao jana wametakata pale Chamazi. Ushindi ambao unawafanya gap la point liwe point 14 huku Simba wakiwa na faida ya michezo miwili ,hii pia maana yake endapo atashinda michezo hiyo miwili kwa kuanzia huu wa leo basi gap la point litakuwa 8. 
Rally Bwalya akiwaacha wachezaji wa Coastal Union Hance Masoud (22) na Abdul Seleman Sopu.

Kuruhusu kupoteza mchezo leo au kukosa point anagalau moja kati mchezo huu ni kuuweka ubingwa wao rehani mbele ya mpinzani wao mkubwa Yanga anayeashiria kujipanga vyema msimu huu.

Kwa upande wa ‘Wanamagushi’ambao wamerudia majukumu ya benchi la ufundi kwa Kaka yangu Juma Mgunda toka kwa Melis Medo atatakiwa achange karata zake vizuri sana katika mchezo huu.

Kwa kuwa mazingira ya timu hayapo vizuri hadi sasa michezo 18 point 21 magoli ya kufunga 14 na yakufungwa 20 nafasi yao ni ya 12 miongoni mwa timu 16 hivyo unajiona majaliwa yao ya kubaki msiimu ujao yanahitaji mapambano makubwa ikiwemo kushinda game za aina hii.

Shomari Kapombe akijaribu kuupiga mpira mbele ya mlinzi wa Coastal Union.

Hapo ndiyo nauona ugumu wa mechi unavyoenda kuwa jioni ya leo hii wenyewe wanasema ‘hakuna kulala hakuna kuremba’.
Kikosi cha sasa cha Coastal pamoja na kuwa na wachezaji wakigeni maarufu kama Mapro zaidi ya wanne ndani ya kikosi hicho bado wanamtumaini zaidi kama si kumtegemea Bwana mdogo Hamis Seleman Sopu.

Dirisha dogo wameondokewa na wachezaji kadhaa wa wa kikosi cha kwanza akimo Issa Abushehe,Hamad Majimengi Hance Masoud. Japo mtu kama Ayub Semtawa Aman Kyata wamepandisha sana viwango vyao lakini kiukweli wanakazi kubwa dhidi ya Lunyasi leo.

Kwa upande wa Lunyasi wao wamekuwa motivated na kufuzu hatua ya robo fainali ya kombe la shirikisho wataingia katika mechi hii wakiwa na uhitaji mkubwa wa point 3.

Sambaza....