Yanga wanashuka katika uwanja wa Benjamin Mkapa kuwakaribisha Rivers United katika mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika katika hatua ya robo fainali.
Yanga wanakwenda kuingia katika mchezo wa kuamua historia ya maisha yao katika soka la Kimataifa kwani kufuzu kwao kwenda nusu fainalo itakua ni mara yao yakwanza kutinga hatua hiyo katika michuano mikubwa ya Afrika.
Ndio ni mara yao yakwanza kwani walishawahi kucheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 1998 lakini hawakuvuka hatua hiyo na hayo yanabaki kuwa mafanikio makubwa ya katika ngazi ya Kimataifa.
Kitu kizuri kwa Yanga leo ni kwamba wanaingia katika mchezo wa historia yao huku wakiwa na faida ya ushindi wa mabao mawili kwa bila walioupata ugenini Nigeria hivyo ni wazi hesabu za Yanga mpaka sasa zinaenda vyema upande wao.
Tayari kocha Nabi alishasema wameshasahau matokeo yaliyopita ya mchezo wa awali hivyo wanaweka asilimia 100 katika mchezo waleo, wakati Zawadi Mauya yeye alisema watapambana mpaka mechi ya mwisho ndio watafahamu wameweka historia gani katika klabu yao.
Kweli ni siku ya maisha yao lakini Wananchi bado wanapaswa kuwa makini na dakika 90 zilizobaki ili kuandika historia kwani kwenye mpira lolote linaweza kutokea. Wanapaswa kukumbuka jinsi watani zao Simba walipotolewa na Jwaneng Galaxy msimu uliopita.