Sambaza....

Wachezaji wawili wa timu ya Taifa ya Russia Aleksandr Kokorin wa Zenit St Petersburg na Pavel Mamaev wa Krasnodar wapo katika uchunguzi kufuatia tukio la kumpiga mtumishi wa uma kwenye Mgahawa wa chakula mjini Moscow.

Wachezaji hao wanatuhumiwa kwa kumpiga mfanyakazi wa wizara ya Biashara Denis Pak na kumsababishia majeraha yaliyomuhitaji kupatiwa matibu na tayari Wizara ya mambo ya Ndani imefungua uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.

“Kwa sasa tayari uchunguzi umeshafunguliwa, na utahusisha hali zote na wahusika wote waliokuwapo kwenye eneo la tukio,” Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani imesema.

Tayari Klabu ya Zenit imetoa taarifa na kusema kuwa Kokorin amewafadhahisha huku klabu ya Krasnodar ikiripotiwa kuwa katika mpango wa kusitisha mkataba wa Mamaev kutoka na kitendo hicho.

Kokorin mwenye umri wa miaka 27 ameichezea mechi 48 timu yake ya Taifa lakini hakuwepo kwenye michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika nchini Russia kutoka na kuwa na majeraha lakini amekuwa akiitumia klabu ya Zenit toka mwaka 2016.

Kwa upande wake Mamaev mwenye umri wa miaka 30 ameichezea Russia mechi 15, pia kabla ya kujiunga na Krasnodar mwaka 2013 alikuwa akiitumikia CSKA Moscow ambapo alicheza mechi 128.

“Kwa sasa tunaangalia namna bora ya kuvunja mkataba na Mamaev, kwa bahati mbaya mikataba imetengenezwa kwa kuwalinda wachezaji katika hali kuwa zaidi, lakini tutafanya vyovyote kuhakikisha hilo linatokeo,” taarifa ya klabu ya Krasnodar imesema.

Sambaza....