Tovuti ya Kandanda ilipata nfasi ya kufanya mahojiano mtandaoni na mlinzi wa Tanzania anayechezea klabu ya Baroka FC ya nchini Afrika kusini. Haya ni maswali yetu ambayo tulimuuliza tumekuwekea hapa uweze kuyapata pia.
Historia yako fupi mpaka kufikia hapo Baroka
Kwa kifupi, nilianzia Kombezi Academy kwa mwalimu Khalfan Kamote ndio aliegungndua kipaji changu ndio nikahamia Uruguay baadae African Sports then (harafu) Coastal Union nikaenda Simba Cc mpk hapa nilipofikia
Changamoto zipoje tanguulipofika Baroka kwa mara ya kwanza?
Sijakutana na changamoto zozote kwa sababu mpira wa huku upo wazi, mwenye kufanya vizuri mazoezini ndio anacheza mechi.
Tofauti ni ipi kati ya Simba na Baroka
Sio simba tu Tanzania bado tupo nyuma sana, lakini kwa uongozi uliokuwepo sasa kila kitu kitakuwa sawa taratibu
Hata ukifatilia ligi ya huku (ABSA League) msimamo wao utaona tofauti sana.
Unazikabiri vipi changamoto za maisha hasa kwenye suala la ubaguzi? (Nje ya mpira)
Huku hakuna ubaguz kuanzia uwanjani timu pinzani hata mazoezini na maisha ya kawaida hakuna ubaguzi.
Umejifunza nini kwenye mpira wa Afrika kusini
Kwa mpira huku wanauchukulia serious na unachezwa uwanjan sio kwenye media na mpira wa huku una speed (Kasi) sana na vingi nimejifunza nikiorodhesha hapatatosha
Tanzania kumekuwa na malalamiko mengi kuhusu waamuzi hili lipoje kwenye ligi ya Afrika kusini?
Huku waamuzi wanakosea sana kuliko Tanzania lakini hakuna mtu anaelalamika baada ya mechi au media (vyombo vya habari) kuzungumzia sababu muamuzi ni binadamu.
Na tanzania waaamuzi wanakuwa wabaya pindi Simba na Yanga zikifungwa tu au nakosea? Lakini huku yoyote anafungwa iwe nyumbani au ugenini.
Umeridhika na hapo ulipo kama bado je mipango yake ipoje na unataraji kuelekea wapi?
Mimi nipo chini ya kampuni ya Siyavuma Group wao ndio kazi yao kunotafutia timu mm kazi yangu kucheza tu kokote kwasasa sina mamlaka ya kujua ntakuwepo hapa msimu ujao au lah.
Ni kweli umeingia mkataba na Adidas? unanufaika vipi.
Navalishwa na adadis viatu nimetafutiwa mkataba na kampuni inayonisimamia ili iwe rahisi kucheza mpira na wananilipa vizur kwa miaka miwili.
Ushauri gani kwa wachezaji wanaocheza hapa ili waweze kucheza nje ya Tanzania?
Wawe na wivu wa maendeleo na wakubali kuwa wajinga ili wajifunze zaid