Sambaza....

Michezo ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika imemalizika rasmi Jumamosi na tayari vilabu vinne vitakavyocheza nusu fainali vimeshafahamika wakisuburi tu wakati wa mitangange hiyo kupigwa.

Timu nne zilizofuzu ni Wydad Casablanca, Al Ahly, Esperence de Tunis zote kutoka Afrika Kaskazini na Mamelodi Sundowns kutoka Afrika Kusini, wakiwaacha Simba Sc, CD Belouzdaid, Raja Casablanca na JS Kabyele zikiaga mashindano.

Wydad wao waliiondosha Simba kwa mikwaju ya penati baada ya sare ya bao kwa moja, Mamelody alishinda ushindi wa jumla wa mabao 6-2 dhidi ya Belouzdai, Ahly yeye amemtoa Raja kwa ushindi wa mabao mawili kwa bila na Esperance walipata ushindi wa bao 2-1 dhidi ya JS Kabyele.

Wachezaji wa Simba wakati wa upigani mikwaju ya penati katika mchezo dhidi ya Wydad Casablanca.

Kandanda inakupa thamani ya vikosi vyote kwa mujibu wa mtandao wa Transfermarket  ambavyo vimefuzu kucheza nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, mashindano makubwa kwa ngazi ya Klabu Barani Afrika kwasasa.

Esperance de Tunis

Wababe hawa kutoka Tunisia wamefuzu nusu fainali kwa kuwatoa JS Kabyele baada ya ushindi ugenini na sare nyumbani. Kikosi hicho cha Esperance kina thamani ya € milioni 18.7 ambayo ni takribani bilioni 44.8 za Kitanzania.

Katika kikosi hicho kina wachezaji nane wakigeni huku waliobaki wakiwa ni wazawa na wanaoitumikia timu ya Taifa ni 10. Mchezaji mwenye thamani kubwa ni mlinzi wao wa kati Mohamed El Be mwenye thamani ya €2.5 milioni.

Esperance de Tunis

Wydad Casablaca

Wababe wa Simba hawa baada ya kufuta za ndoto za Mnyama kucheza nusu fainali kwa kuwaondosha kupitia mikwaju ya matuta. Kikosi cha Wydad kutoka nchi ya Morocco  Afrika ambayo ndio Taifa pekee limecheza nusu ya kombe la Dunia ina wachezaji sita wa Timu ya Taifa ikiwa na wachezaji watano pekee wakigeni.

Thamani ya Wydad Casablanca ni €19.5 sawa na bilioni 46.8 kwa fedha za Kitanzania kikiwa na mlinzi wa pembeni Yahiya Fatia akiwa mchezaji ghali mwenye thamani €2.5 milioni.

Wydad Casablanca.

Mamelody Sundowns

Masandawana au “The Brazilians” unaweza ukawaita hivyo, wababe wa hatua ya robo fainali hawa kwani wametoa CD Belouzdaid kwa mabao sita kwa mawili, ndio timu pekee iliyoshinda nyumbani na ugenini hatua hii.

Mamelody ina thamani ya €27.30 milioni sawa na zaidi ya bilioni 65.5 kwa Shilingi za Kitanzania wakiwa na wachezaji tisa wakigeni na 13 wanaocheza timu ya Taifa ya Afrika Kusini. 

Mchezaji ghalo kabisa katika kikosi hicho cha “The Brazilians” ni raia wa Chile anaecheza eneo la kiungo ni Marcello Alende mwenye thamani ya €2.00 milioni.

Mamelodi Sundowns “Masandawana”.

Al Ahly

Mashetani Wekundu wa Misri hawa wamewatoa Raja Casablanca kwa mabao mawili kwa sifuri kama ambavyo walifanya mwaka jana. Al Ahly kikosi chao kina thamani ya €29.55 sawa na kama bilioni 70 za Kitanzania, ndio kikosi ghali zaidi katika hatua hii.

Ahly wana wachezajo wakigeni sita na wachezaji nane waliopo timu ya Timu ya Taifa huku ni mlinda mlango Mohamed El Shanawi mwenye thamani zaidi akiwa amethaminishwa kwa kiasi cha €2.5 milioni. 

Al Ahly “Red Devils”

Kwa Upande wa Simba

Kwa mujibu wa Transfermarket kikosi cha Simba kina thamani ya €1.93 ambayo ni takribani bilioni nne kwa pesa ya Kitanzania. Ni dhahiri shahiri Simba wanapaswa kutanua msuli na kuendelea kuongeza bajeti yao katika usajili ili kuweza kupambana na vigogo wa Afrika. 

 

Sambaza....