Zanzibar ndiyo ilikuwa sehemu yao ya kwanza kuanza safari yao na Ethiopia ikawa safari yao ya mwisho kwenye michuano hii ya kimataifa.
Walifanikiwa kutoka sare ya goli moja kwa moja dhidi ya Zimamoto ya Zanzibar katika uwanja wa Amani na walippenda kurudiana Ethiopia walifanikiwa kuwafunga Zimamoto goli 1-0 na kufanikiwa kufuzu hatua ya kwanza ya kombe la shirikisho barani Afrika.
Tanzania itanufaika vipi Yanga ikifuzu hatua ya makundi CAF?
Ambapo walienda kukutana na Zamaleki ya nchini Misri, Zamaleki ambayo ina historia kubwa ya mashindano ya vilabu barani Afrika lakini walifanikiwa kuwatoa kwa changamoto za mikwaju ƴya penalti baada ya mchezo wa kwanza nchini Ethiopia kushinda magoli 2-1 na walipoenda Misri , Zamaleki walishinda 2-1 timu zikaenda katika changamoto za mikwaju ya Penalti ambapo Walayta Dicha walifanikiwa kupita na kukutana na Yanga ambayo ilitokea katika michuano ya klabu bingwa Afrika baada ya kutolewa na Township Rollers.
Licha ya kipigo cha bao moja kutoka kwa Welayta Dicha ya Ethiopia timu ya Yanga imetinga hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho Afrika kwa jumla ya mabao 2-1.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 ambao umesaidia kuivusha hatua hiyo.
Dicha walianza kwa kasi mchezo huo na walipata bao la mapema dakika ya pili kupitia mshambuliji wao tegemeo Arafat Djako.
Yanga ilicheza mfumo wa kujilinda zaidi ikimuacha Obrey Chirwa peke yake mbele akikabwa na walinzi wanne.
Kwa kuingia hatua hiyo Yanga itavuna zaidi ya sh milioni 600 za maandalizi zinazotolewa na Shirikisho la mpira wa miguu Afrika (CAF).