Sambaza....

Hatimae hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika imetamatika na timu nane zitakazocheza robo fainali zimefahamika huku nyingi zikiwa ni kutoka nchi za Kiarabu Afrika Kaskazini.

Katika timu nane kutoka makundi yote manne timu sita zinatoka Afrika Kaskazini katika nchi za Tunisia, Misri, Algeria na Morocco wakati timu moja inatoka Afrika ya kusini na moja mashariki.

 

Timu nne zilizoongoza makundi yao ni hizi hapa Waydad na Raja Casablanca (Morocco), Esperence de Tunis (Tunisia) na Mamelody Sundows (Afrika Kusini). Timu zilizomaliza nafasi ya pili JS Kabyele na CD Belouzdaid (Algeria), Al Ahly (Misri) na Simba Sc kutoka Tanzania.

Droo ya robo fainali inatarijiwa kupagwa hivi karibuni wakati michezo ya robo fainali inatarajiwa kupigwa April 21/22 na michezo wa marudiano kupigwa April 28/29 mwaka huu.

Mamelody Sundows “Masandawana” 

Kwa upande klabu ya Simba wao wamemaliza nafasi ya pili katika kundi C hivyo wanaweza kukutana na washindi wa kwanza wa makundi mengine, hivyo Simba huenda akakutana na Mamelody Sundons, Wydad Casablanca au Esperence de Tunis.

Simba itampasa kuchanga vyema karata zake katika mchezo wa kwanza kama kweli wanataka kwenda nusu fainali kwani wataanzia nyumbani mchezo wa kwanza na kumalizia ugenini mchezo wa mwisho.

Sambaza....