Sambaza....

Unaikumbuka YOU WILL NEVER WALK?, Wimbo wenye ambao huleta matumaini mapya katika uwanja wa An field?, vipi kuhusu TO DARE IS TO DO? ya Tottenham Hotspur?

Na hii ya Manchester United ?”Theatre of Dreams” haya ni maneno matatu mazito ambayo lazima ukutane nayo kila unapoingia katika mlango wa Manchester United.

Klabu kubwa duniani, klabu tajiri duniani na ndiyo klabu yenye mashabiki wengi duniani na kwa kifupi unaweza kuiita hii ndiyo klabu inayopendwa sana duniani.

Imechukua mioyo ya watu wengi sana duniani na hii ni kwa sababu tu ya mafanikio makubwa ambayo yanapatikana katika klabu hiyo.

Hakuna biashara ngumu na yenye pesa nyingi duniani kama biashara ya kuuza hisia. Hii ndiyo biashara yenye pesa nyingi sana.

Ndiyo biashara ambayo huwafanya wanunuzi kuwa wafuasi. Ni jambo la kawaida sana kumkuta mteja wa bidhaa Fulani kageuka kuwa mfuasi.

Na hii ni kwa sababu moja tu, muuzaji kafanikiwa kwa kiasi kikubwa kuiuza bidhaa yake kwa kuweka nakshi inayoitwa hisia ndani ya bidhaa yake.

Watu huona kama bidhaa husika imebeba sehemu kubwa ya maisha yao. Wengine huona bila bidhaa hiyo hawawezi kutosheka mahitaji yao.

Hapa ndipo Manchester United walifanikiwa. Walianzia hapa. Walifikiria namna ya kuuza hisia kwa watu wanaopenda mpira duniani.

Wakafanikiwa kwa kiasi kikubwa sana, wakawa na mashabiki wengi sana kila kona ya dunia. Mashabiki ambao wamegeuka kuwa wafuasi wa bidhaa ya Manchester United.

Ni wafuasi haswa, tena sana ndiyo maana kuna wakati Real Madrid walikuwa wanabeba ligi ya klabu bingwa barani ulaya lakini klabu tajiri zaidi ilikuwa inabaki kuwa Manchester United.

Wafuasi wa Manchester United walinunua bidhaa za klabu zao kwa moyo kwa sababu wanaipenda timu kutoka moyoni. Timu yao ni nusu ya maisha yao.

Haya yote yalianzia kwenye falsafa hii ya THEATRE OF DREAM’S. Hapa ndipo penye uchawi mkubwa wa mafanikio ya Manchester united.

Kila mchezaji aliyekuwa anakanyaga kwenye ardhi ya Manchester United, alijua yupo kweye jumba la ndoto, ndoto isiyoisha , ndoto yenye mwendelezo, ndoto ya kuwa na mataji mengi sana.

Ndiyo maana Manchester United ilishinda makombe mengi, na siyo kushinda tu, walishinda kwa hisia kubwa hisia ambayo ilikuwa inatangazwa sana kila timu ikishinda.

Masikio yatasikia mahubiri ya mafanikio ya Manchester United na masikio yalivyo yatashawishi moyo kuipenda Manchester United.

Falsafa ni kitu muhimu sana kwenye biashara yoyote yule ili ufike mbali. Falsafa ina nafasi kubwa ya kumfanikisha mfanyabiashara auze hisia kwa wateja wake kwa kiasi kikubwa.

Simba Sc msimu huu wamekuja na falsafa nzuri sana kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika hatua ya makundi.

Falsafa ya YES WE CAN. Najua falsafa hii ilikuwa mahususi sana kwa ajili ya kuwaonesha wale ambao walikuwa hawana imani ya Simba kufanya vizuri kwenye hatua hii ya makundi.

Ndiyo maana baada ya vipigo vizito kutoka kwa As Vita na Al Ahly falsafa hii imepungua sana na kuna wakati mwingine wanaogopa sana kuitumia.

Ñatamani sana Simba wanisome hapa na kunielewa kipi ambacho nataka kuwashauri. Turudi nyuma kwenye uuzaji wa hisia pamoja na mfano ambao nilioutoa kuhusu Manchester United.

Mafanikio ya Manchester United yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na hii falsafa yao ya THEATRE OF DREAM’S. Ndiyo maana wamefanikiwa sana.

Na hapa ndipo kuna nafasi kubwa ya Simba wao kutumia YES WE CAN kama falsafa yao na wakafanikiwa kuitumia kwa muda wote na ikawa kitu ambacho kitawanufaisha sana.

Kwanza kila kizazi ambacho kitapita Simba kitajengewa mazingira ya kujiamini kuwa kinaweza kufanya kitu chochote kikubwa kupitia kampeni ya YES WE CAN.

Washabiki wa Simba Uwanjani

Na ndipo hapo panaweza pakawa mwanzo wa kupandisha morali ya wachezaji kufanya vizuri na kufikia hatua kubwa ya mafanikio ya soka.

Ushajiuliza jinsi ambavyo itawanufaisha kibiashara?, kuna wakati viongozi wa klabu huitaji morali ndani yao.

Morali ambayo itawakumbusha kipi wanatakiwa kukifanya ndani ya klabu ?, ndipo hapo umuhimu wa YES WE CAN unapokuja.

Kivipi?, kila kiongozi atakayeingia atafikiria kuanzisha au kubuni kitu chenye faida kubwa kibiashara na hiki kitu kitasukumwa na nguvu ya falsafa hii ya YES WE CAN.

Hakutakuwepo na moyo wa kukata tamaa kwa kuamini kuwa falsafa yao inatoa nguvu kubwa sana. Kwa mashabiki vipi?

Kampeni hii inaweza kuwa na faida kubwa kwa mashabiki ndani na nje ya uwanja. Kivipi?, tuanze na ndani ya uwanja.

Kupitia falsafa hii mashabiki wataingia uwanjani kuipa nguvu timu yao kwa kuamini kupitia hiki kitu YES WE CAN.

Wataisimama kwenye jukwaa wataimba wimbo huu wa YES WE CAN kwa nguvu kubwa sana na kuwakumbusha wachezaji kuwa wasikate tamaa.

Hata nje ya uwanja mashabiki watakuwa na nguvu ya kununua bidhaa za vilabu vyao kwa kuchagizwa na falsafa hii ya YES WE CAN.

Sambaza....