Sambaza....

Klabu ya Manchester United ipo tayari kuachana na wachezaji na nyota wake 13 kuelekea usajili ujao ili kutengeneza nafasi kwaajili ya nyota wapya wanaotakiwa na kocha wao Erick Ten Hag.

United imepanga kuachana na wachezaji hao akiwepo pia nahodha wake Harry Maguire ili kupunguza mishahara mikubwa wanayotoa lakini pia kufanikisha kusajili wa wachezaji wengine watakaoendana na mfumo wa Harry Maguire. 

 

Miongoni mwa nyota wanaotajwa kuachwa ni pamoja na Erick Bailly, Alex Telles na Brandon Williams waliopo nje kwa mkopo, wakati pia majeruhi na kutokuelekewa kwa viwango vya Van de Beek na Anthony Martial kunawafanya kuwa katika nafasi ya kuachwa pia.

Mlinzi wa pembeni Aroon Wan Bisaka, nahodha Harry Maguire na mshambuliaji Anthony Elanga nao wapo tayari kuonyeshwa njia ya kutokea ili kuwapa nafasi nyota wapya watakaosajiliwa katika usajili huu.

Miongoni mwa nyota wanaohusishwa kuhamia Old Traffod ni pamoja na mlinzi wa pembeni wa Bayern Levekursen Jeremi Frimpong, mshambuliaji wa Napoli Victor Osimhen ama nahodha wa Spurs Harry Kane. 

Kocha wa United baada ya kuanza msimu vyema na kuwa na matarajio makubwa ya kufuzu Ligi ya Mabingwa ameonekana kutaka kuendelea kuijenga na kuiimarisha United kwa kuongeza wachezaji watakaendana na falsafa zake na ukubwa wa United.

Sambaza....