Sambaza....

Nyota wa Kimataifa wa Tanzania anaekipigika katika kikosi cha JS Souara cha nchini Algeria amejikuta katika wakati mgumu akiwa uwanja wa Taifa alipokua akikabiliana na Simba katika hatua ya makundi ya klabu bingwa Africa.

Katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Klabu Bingwa Africa Ulimwengu na timu yake walikubali kipigo cha mabao matatu kwa sifuri katika uwanja wa Taifa wa jijini Dar es salaam. Js Souara kwa matokea hayo yanawafanya waburuze mkia baada ya ushindi wa Al Ahly wa mabao mawili dhidi ya As Vita.

Msimamo wa kundi D baada ya michezo ya jana.

Thomas Ulimwengu alionja joto ya uwanja wa Taifa baada tu yakukanyaga nyasi za uwanja wa Taifa baada ya kupata wakati mgumu kutoka kwa mashabiki na wachezaji wa Simba.

Ulimwengu alipoingia tuu uwanjani ili kupasha misuli mashabiki wa Simba walisikika wakimzomea kwanguvu bila kuchoka, lakini Ulimwengu alifunga vioo bila kujali na kuendelea na program za timu kama kawaida mpaka waliporudi vyumba vya kubadilishia nguo.

Hata alipoingia dakika ya 57 mashabiki waliendelea kumzoea ili kumtoa mchezoni mchezaji huyo wa zamani wa TP Mazembe. Mashabiki pia waliendelea kufanya hivyo hata akiwa uwanjani huku kila akigusa mpira alikua anazomewa.

Uwanjani pia aliendelea “kuteseka” baada ya kudhibitiwa vilivyo na Mohamed Hussein aliekua nahodha katika mchezo huo. Ulimwengu aliekua anacheza upande wa kulia alijikuta akimilikiwa vizuri na Tshabalala na kushindwa kuleta madhara yoyote katika lango la Simba na kushindwa kuisaidia timu yake kuepuka kipigo.

Mpaka mpira unamalizika Thomas Ulimwengu alikua “anateseka” na kuzomewa na mashabiki wa Simba na pia alikikuta “anateseka” na matokeo ya kipigo cha mbwa koko cha mabao matatu kwa bila kutoka kwa Simba sc.

Ulimwengu amebaki na kibarua kingine kigumu cha kuipigania timu yake na kuitoa mkiani wakiwa nyumbani kuikaribisha Al-Ahly ya Misri katika uwanja wa wao wa nyumbani. Al-Ahly wao wanashika nafasi ya pili katika kundi D baada ya kuifunga AS Vita.

Sambaza....