Sambaza....

Kesho Klabu ya Simba itacheza na Association Sportive Vita ( As Vita) katika uwanja wa Stade des martyrs wenye uwezo wa kubeba mashabiki 80,000.

Mechi za mkondo wa kwanza , Simba alishinda nyumbani goli 3-0, wakati As Vita alifungwa ugenini goli 2-0. Zifuatazo ni sababu ambazo zinaonesha kwanini As Vita ana nafasi kubwa ya kushinda mechi ya kesho.

UWANJA WA NYUMBANI.

As Vita wamekuwa na matokeo mazuri sana katika uwanja wao wa nyumbani. Kwa mfano katika mechi 10 zilizopita ambazo wamecheza nyumbani, hawajafungwa hata mechi moja, huku wakitoa sare mchezo mmoja na kushinda michezo 9.

Pia safu yake ya ushambuliaji ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani imekuwa hatari sana. Kwa mfano kwenye hizo mechi kumi zilizopita ambazo As Vita kacheza nyumbani amefunga magoli 20.

Magoli 20 katika mechi 10 ni wastani wa kufunga magoli 2 katika kila mechi. Huku wakifungwa magoli 5 tu katika mechi 10 walizocheza nyumbani.

Kuna faida ya mashabiki katika uwanja wao wa nyumbani ?

Shabiki ndiye mchezaji wa 12 kwenye timu kwa hiyo As Vita watakuwa na nafasi kubwa ya kunufaika na mashabiki wake katika uwanja wao wa nyumbani.

UZOEFU WA MASHINDANO YA CAF.

As Vita ina uzoefu mkubwa na imefanya vizuri zaidi katika michuano ya CAF kuzidi klabu ya Simba. Hivo wanajua jinsi ya kucheza kwenye michuano hii ya CAF.

Msimu jana walifika fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Raja Casablanca na wakafungwa katika fainali.

Hii inaonesha dhahiri kuwa As Vita ni moja ya timu ambazo zinajua jinsi ya kupata matokeo chanya katika michuano hii ya CAF kutokana na mafanikio ambayo wanayapata.

SAFU YA ULINZI YA SIMBA.

Simba katika michezo 6 iliyopita, Simba amefungwa magoli 6, ikiwa ni wastani wa kufungwa goli moja kwa kila mechi.

Na As Vita katika uwanja wao wa nyumbani wana wastani wa kufunga goli 2 kwenye kila mechi kwa mechi 10 zilizopita.

Na katika michezo 10 iliyopita waliyocheza nyumbani ni mchezo mmoja tu ambao hawajafunga goli.

Wanakutana na timu ambayo ina wastani wa kufungwa goli 1 kwenye kila mechi kwa mechi 6 zilizopita.

Sambaza....