Sambaza....

Kampuni ya promosheni ya ngumi Mo Green Promotion leo imetambulisha mapambano ya ngumi yatakayofanyika mkoani Mwanza mapema July mwaka huu ikijulikana kama Mo Strong Vitasa Night.

Mratibu wa mapambano hayo Kessa Mwambeleko amesema mabondia ghali na maarufu nchini watapanda ulingoni kunogesha shughuli hiyo itakayofanyika Mwanza katika ukumbi wa Malaika.

“Tutakua na mapambano ya ngumi katika siku ya Mo Green Vitasa Night ambapo Twaha Kiduku atapambana na bondia kutoka Afrika Kusini Asemahle Welemjina na Karim Mandonga nae atapigana na bondia kutoka Uganda Moses Golola,” alisema na kuongeza

“Kutakua na mapambano nane yaani manbondia 16 watapanda ulingoni na tunampango wakupngeza wengine. Kwa mara ya kwanza watu wa Mwanza watapata nafasi ya kuwaona Karim Mandonga na Twaha Kiduku kwa pamoja. Pia kutakua na mziki wa bendi hivyo watu wa Mwanza watapata burudani za ngumi pamoja na muziki. Utakua ni usiku wa aina yake kwa watu wa Mwanza.”

Karim Mandonga (katikati).

Kwa upande wa bondia Twaha Kiduku anaetarajiwa kupambana pambano la main card alisema “Ninashukuru kupata pambano hili, nawashukuru Mo Green. Ninaendelea kufanya mazoezi ili kumdondosha Msauzi, mashabiki mje kwa wingi sitawaangusha mambo ni “show show” tuu nitakuwa na kaka yangu Mandonga.”

Ukiachana na pambano la main card pia Karim Mandonga atapanda ulingoni kupambana na Mganda Moses na kuelekea pambano hilo Mandonga amekuja na ngumi inaitwa “Ndukube”.

“Nitakua na mdogo wangu Kiduku namkubali sana na nafurahia sana tumepata fight kubwa Jijini Mwanza nikiwa nae. Sasa huyu Mganda nitambatiza jina jipya, yule wa mwanzo nilimbatiza kulekule kwao.  Sasa fanya mambo yako yote usikose kuja Mwanza nina ngumi mpya inaitwa Ndukube hiyo ukipigwa na mkono wa kulia unageuka kichuguu, ukipigwa na kushoto unapata fangasi.”


“Hii ngumi inatoka mbali inatoka msitu wa Mbambadu, yanu mtu atoke kwao aje kutamba kwako!?

Pambano hilo katika upande wa afya za mabondia na usalama wa ulingo utakua chini ya usimamizi wa duka la dawa. Ambao wao watawapima mabondia, watawacheki afya zao wakitumia timu yenye wataalamu yakinifu.

Sambaza....