Sambaza....

Soka la wachezaji wetu wa ndani kwa maana ya viwango vyao limeshuka sana kulinganisha na msimu mmoja uliopita.

Kwa asilimia kubwa baadhi tu ya wachezaji wa kigeni viwango vyao vipo vizuri lakini wengi pia vipo chini kutoa mfano bora na ushindani kwa wazawa.

Hii ni hatari kwa timu yetu ya taifa . Ubora wa timu yetu ya taifa kwa ‘ pool ‘ kubwa ya wachezaji wa ndani itaathirika vibaya kwa michuano iliyo mbele yetu.

Lazima Shirikisho kwa maana ya kitengo cha ufundi kufuatilia vyema hili.

Msimu wa 2016-17 na 2017-18 wazawa wengi walikuwa wazuri na kuleta ushindani mzuri . Kumbuka michuano ya COSAFA kule SA na baadhi ya mechi chini ya mzee Salumu Mayanga .

orodha ya wafungaji bora

Kina Dante , Kichuya , Mzamiru , Keny Ally , Bocco , Kiyombo , Mussa wa JKT tangu afungane ufungaji bora na Msuva kapotea hata kwenye headlines, Bocco ndio soka linakwenda alijojo na ndio tegemeo kwenye safu ya ushambuliaji…oooh wachezaji wengine mpaka wameshushwa madaraja ya chini mfano Mbaraka Yusufu wa Azam FC kwenda Namungo FC inayoshiriki ligi daraja la kwanza .

Beno Kakolanya

Makosa ya kinidhamu kwa Beno Kakolanya na hukumu aliyopewa na klabu yake ya Yanga ni pigo lingine kwa Taifa Stars na soka letu kwa ujumla. Simuoni kipa mwingine wa kumpa ‘ challenge ‘ Aishi Manula pale Taifa Stars pia ubora wa kumkaribia endapo ataumia au kupata shida yoyote ile .

Naliona soka la ndani kudidimia kwa kasi kubwa licha ya idadi kubwa ya vijana wetu chipukizi kujaribu bahati zao nje .

Mfungaji Bora mwezi wa Tisa wa ligi Kuu Tanzania bara, Eliud Ambokile, akiwa na zawadi yake kutoka katika tovuti ya kandanda ya kumpongeza.

TFF ni lazima ije na malengo ya miaka 5 mpaka 10 kuimarisha soka la ndani ili kupata ‘ pool ‘ kubwa ya wachezaji wazawa wenye ubora mzuri .

Vijana waliofanya vizuri na Serengeti boys wengi wao wanapotea sasa kwa kukosa mwendelezo mzuri . Kina Mkomola , Buruani na wengineo siwaoni kupata breakthrough sahihi kisoka ili taifa livune matunda yao.

-Makala hii imeandaliwa na Samuel Samuel

Sambaza....