- Safari ya Yanga, Mikononi mwa Dube
- Simba na Yanga nani anaongoza kuweka mpira kwapani.
- Yanga Waweweseka! Gamondi Nje!
- Fadlu Tunaamini anawapa Ubingwa Wekundu
- Manuel Neuer ana umri sawa na uchambuzi wa soka kwa kompyuta
Kabla ya mechi Barcelona haikuzungumzwa sana kama ambavyo Lionel Messi alivyozungumzwa na watu wengi.
Huyu ndiye ambaye alionekana kama mtu ambaye angeweza kwa kiasi kikubwa kuwaangamiza Manchester United.
Na siyo kuwaangamiza pekee, ila kung’ara kuzidi mchezaji yeyote ndani ya uwanja. Haya ndiyo mategemeo ya watu wengi.
Mategemeo ambayo yalikuwa karibu kabisa na ukweli. Hapana shaka lionel Messi amekuwa mchezaji hatari ndani ya miaka 10 iliyopita.
Amefanikiwa kudumu kwenye kiwango chake, hajatetereka kiasi cha kuanguka kabisa, hajawahi kuwa chini kwa muda mrefu.
Amesimama kama mchezaji aliyekomaa zaidi kimaamuzi ndani ya muongo mmoja uliopita. Na amesimama kama mchezaji bora zaidi ndani ya muongo mmoja uliopita.
Na amekuwa mhimili mkubwa sana ndani ya timu ya Barcelona. Kwa miaka ya hivi karibuni ilikuwa ngumu kuitaja Barcelona bila kumtaja Lionel Messi.
Na kwa msimu huu anaonekana ndiye ameibeba Barcelona. Magoli 43 ndani ya michezo 40 ndani ya msimu huu yametoka kwenye mwili wake.
Miguu yake imefunga, kichwa chake kimefunga na ndani ya mechi 6 zilizopita amefunga goli 6 wastani wa kufunga goli moja kwenye kila mechi.
Kwa kifupi kabla ya kukutana na Manchester United huyu ndiye ambaye alikuwa anatazamiwa kuwa nyota wa mchezo huu kwenye uwanja wa Old Trafford.
Ukiachana na pasi ya mwisho ya goli la Luiz Suarez aliyoitoa hakuna ƙkingine kikubwa ambacho alikifanya jana kwenye mechi ambayo alitegemewa kufanya makubwa.
Unajua kwanini ?, uwepo wa Scott McTomminay, huyu ndiye ambaye alifanikisha Lionel Messi kutong’ara sana kwenye mechi hii.
Huyu ndiye ambaye alikuwa anamu PRESS sana Lionel Messi kila akipata mpira katika eneo la katikati mwa uwanja katika mechi ya jana.
Huyu ndiye ambaye alikuwa anahakikisha anaghasi ghasi Lionel Messi ndani ya uwanja. Hakutaka kumwacha akiwa anatafakari chochote.
Kila alipokuwa anajaribu kutafakari chochote kile Scott McTominay aliibuka kwa ajili ya kumwondolea uwezekano wa yeye kutafakari chochote kile.
Huyu ndiye ambaye alimfanya Lionel Messi asiwe huru ndani ya mchezo huu. Alikuwa amekabwa sana kwenye mchezo huu.
Scott McTominay ambaye alifanikiwa kucheza mipira yote ya juu katika mchezo wa jana tena kwa utulivu mkubwa.
Utulivu ambao upo mpaka kwenye paji la uso wake. Anaonekana ni mtulivu sana. Hana shida na mtu , muda mwingi anafikiria namna ya kuweza kufanikiwa ƙkucheza vizuri ndani ya uwanja.
Ndicho alichokifanya kwenye mechi ya jana akifanikiwa kucheza vizuri sana. Huyu ndiye mchezaji ambaye hakutazamiwa kung’ara kama ambavyo tulitegemea kwa Lionel Messi