Klabu ya soka ya Yanga imekanusha taarifa zinazoenea juu ya nahodha wake Papy Tshishimbi kuwa amegoma kuichezea miamba hiyo kwa sababu za madai ya maslahi yake.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Klabu hiyo, Hersi Said ameiambia Kipenga ya East Africa Radio kwamba Tshishimbi bado anauguza jeraha linalomkabili na ameanza mazoezi mepesi na si kama inavyoripotiwa.
Kuhusu Mohamed Banka anayeripotiwa kuwa amerejea kwao visiwani Zanzibar akishinikiza malipo yake, Hersi Said amesema hana taarifa juu ya mchezaji huyo ingawa hadai mshahara labda pesa za usajili.
Katika hatua nyingine Hersi amesema kwamba wameshakamilisha mikakati ya usajili kabambe wenye tija utakaoisaidia timu hiyo kurejesha hadhi yake ya kutwaa mataji.
Vilevile amesema upo uwezekano wa Yanga kucheza na Sevilla ya Hispania Katika kilele cha wiki ya mwananchi kwa kuwa tayari wameshaingia makubaliano ya ushirikiano Katika nyanja mbalimbali ya kimichezo