Liverpool anatarajiwa kupambana na Tottenham Hotspurs katika muendelezo wa EPL
ni mechi inayoweza kumtoa nafasi au uelekeo wa bingwa endapo Liverpool watapoteza mchezo huo kwa kuwa wanakaribia sana kitakwimu baina yao na mpinzani wa karibu Man City ambaye ni bingwa mtetezi.
Man City wana alama 83 kibindoni katika michezo 34 huku Liverpool wakiwa na alama 83 michezo 34 kwa maana ya kila upande kubakiza michezo 4 na hata utofauti wa magoli ukiwa ni 1 kwenye GD Liverpool 64 City 63.
Kiukweli ushindani upo pande zote mbili kwenye point na utofauti wa magoli, itakumbukwa kuwa mechi baina yao haikutoa mshindi maana walienda sare ya 2-2.
Kwanini Tottenham anaangaziwa kama ndiyo aliyeshikilia dhamana ya ubingwa wa timu wa msimu huu?
Sababu kubwa ya msingi kwa Spurs kuonekana ni’ mfalme’ katika mechi 8 zilizobaki kwa pande zote mbili ni ubora wao miongoni mwa timu ambazo bado hazijacheza na timu zote mbili.
Liverpool amebakiza na Tottenham, Aston Villa, Southampton, Wolves huku Man City wakibakiza Aston Villa, Westham, Newcastle na Wolve hapo unaweza kupata dhana ya dhamana Spurs kushikilia ubingwa wa msimu huu.
Ikitokea Liverpool kapata matoke ya ushindi ataongoza ligi hadi jumapili wakati City akiwa anacheza na Newcastle. Maana yake nidhamu kubwa ya kupangua mechi moja moja hadi ya mwisho na kumpata bingwa.
Ikitokea kila moja anashinda mechi zake nne zilizobaki basi Man City atakuwa bingwa kwa pointi 95 huku akimuacha Liverpool kwa pointi moja 94 endapo atashinda zote.