Sambaza....

Beki wa kati wa kimataifa wa Tanzania, Abdi Banda, amewataka wachezaji na makocha wa Tanzania kutoka nje ili kujifunza na kuona wenzao wanaendeleaje

Akizungumza na mwandishi wa  tovuti ya Kandanda, Banda alisema kuwa ili kupata timu bora ya taifa kunahitaji kuwa na wachezaji wengi wanaocheza soka nje na ikibidi hata makocha pia.

“Wachezaji wengi watoke nje kucheza ili waone wenzetu wanaendeleaje, pia makocha watafute kazi nje ya Tanzania ili kusaidia vijana na sio kubadilisha timu za bongo tu” alisema mchezaji

Mchezaji huyo wa zamani wa vilabu vya African Sports, Coastal Union na Simba, akusita kuzungumzia suala la waamuzi na kuweka wazi kuwa ata Afrika kusini waamuzi wanakosea sana kuliko Tanzania

“Huku waamuzi wanakosea sana na hakuna mtu anayelalamika baada ya mechi au media kuzungumza sababu muamuzi ni binadamu”

“Na Tanzania waamuzi wanakuwa wabaya pindi Simba na Yanga zikifungwa, huku timu yoyote inafungwa iwe nyumbani au ugenini” aliongeza mlinzi huyo wa Baroka Fc

Mchezaji huyo anayemudu kucheza nafasi nyingi uwanjani, kwa sasa anasukuma kabumbu kunako klabu ya Baroka FC, ya Afrika kusini inayoshiri ligi kuu ya nchi hiyo.

Sambaza....