Sambaza....

Leo Simba itacheza kwenye Sportpesa Cup , atasimama kama mmoja ya wawakilishi wawili waliobaki kwenye michuano hii ya Sportpesa Cup.

Lakini kuna tatizo moja ambalo ni kubwa sana kwenye kikosi cha Simba, tatizo ambalo wanatakiwa kulifuatilia kwa makini sana kama inataka kufika mbali.

Kuna swali kubwa ambalo limezua mjadala mkubwa sana baada ya mechi ya As Vita na Simba. Wengi wanadai kuwa Simba ina mabeki wabovu. Kuna ukweli wowote kuhusiana na kauli hii?.

Tuanzie hapa kwanza.

Simba inajizuiaje ?, ukiitazama Simba ya Patrick Assumes inatumia HIGHLINE DEFENCE, aina hii ya ukabaji ilianzishwa na Arrigo Sacchi. Kocha wa zamani wa Ac Milan ambaye alileta mapinduzi ya soka nchini Italy kwa kuitoa Italy kwenye aina ya uchezaji wa Catannacio na kuleta aina ya ushambuliaji.

Aina hii ya uzuiaji ndiyo inatumiwa sana kwa sasa na Unai Emery , Mauricio Sarri na hapa nchini Patrick Assumes anautumia sana.

HIGHLINE DEFENCE ikoje?, aina hii ya uzuiaji huwataka mabeki wasimame juu kuanzia mita 10-15 kutoka eneo la kipa. Hivo kunakuwa na uwazi mkubwa unaowatenganisha safu ya ulinzi na golikipa. Hapa pia anahitajika kipa ambaye ni Skippers, kipa mwenye uwezo wa kucheza mpira kwa miguu.

Pamoja na kwamba mabeki wanne husimama juu sana, pia husogea mbele kila timu inaposogea. Na hapa safu zote husogea kwa pamoja na kwa karibu karibu.

Kwa mfano, safu ya kiungo inaposogea mbele, safu ya ulinzi hufuata mbele na safu ya kiungo huifuata safu ya ushambuliaji. Hivo zinafuatana kwenda mbele.

Sasa madhara yake ni yapi kwenye timu ?, mpinzani anapopata mpira na kuupenyeza kwa haraka kama ambavyo As Vita walivyokuwa wanafanya huwakuta Simba wakiwa wana uwazi eneo la nyuma.

Aina hii ya uchezaji huifanya Simba kutengeneza SPACES sana eneo la nyuma. Na ndiyo maana asilimia kubwa ya magoli wanayofungwa Simba, mfungaji huwa sehemu ambayo ametumia uwazi uliotengenezwa nyuma.

Hiyo ni moja, mbili mara nyingi mabeki wa Simba wa pembeni huwa wanakuwa juu muda mrefu, na kuifanya Simba iwe na uwazi kwenye eneo la pembeni kutokana na mabeki kukaa juu.

Tatu, viungo wa ulinzi wa Simba hukaa mbali sana na eneo la ulinzi la Simba. Patrick Assumes huitaka Simba icheze juu muda mwingi.

Lakini husahau kuweka tahadhari kwa nyuma , kwa sababu viungo wake wa ulinzi (Jonas Mkude na James Kotei ) hukaa juu muda mwingi, kitu ambacho husababisha gape kati ya safu ya ulinzi na safu ya kiungo cha ulinzi. Hakuna kiungo anayewalinda mabeki wanne wa Simba.

Ndiyo maana timu pinzani ikishambulia kupitia katikati, huwalazimu mabeki wa kati wa Simba , mmoja wao hasa hasa Wawa kuvutika kuja katikati kuziba hilo Gape , na anaposegea huacha space nyuma.

Sasa hapa tatizo ni aina ya uchezaji wa Simba au mabeki ?

Aina ya uchezaji wa Simba wa kufanya HIGHLINE DEFENCE Kimazo ni aina nzuri ya uchezaji , lakini uzuri wa aina ya uchezaji huja pale kocha anapata watu sahihi wa kucheza aina hiyo ya mchezo.

Wachezaji wa Simba hawana uwezo wa kucheza HIGHLINE DEFENCE. Kwanini? Unapotaka timu icheze HIGHLINE DEFENCE , lazima iwe na uwezo wa kufanya HARD PRESSING ikiwa haina mpira.

Hiki kitu Simba hawafanyi ndiyo maana timu ikiwa haina Mpira inakuwa na spaces kwenye eneo lake.

HITIMISHO

Kama Simba wanataka kufanya vyema kwenye michuano hii ya sportpesa na michuano ya CAF lazima kocha awafanye wachezaji wacheze aina ya mpira huu. Timu ijifunze namna ya kufanya HARD PRESSING, Naamini watafanikiwa kufanya HIGHLINE DEFENCE.

Sambaza....