Leo michuano ya Sportpesa imeanza rasmi. Tumeshuhudia timu mbili za Tanzania zikiaga mashindano haya , Singinda United na Yanga.
Kwa Yanga kimekuwa kipigo cha pili mfululizo ndani ya mechi mbili. Kwenye mechi mbili zilizopita Yanga kafunga goli moja pekee na kufungwa goli nne.
Turudi kwenye mchezo wa leo kwenye michuano ya Sportpesa.
Mwalimu mwinyi Zahera alianza na mfumo wa 4-5-1. Huu mfumo ulikuwa wa kujihami sana. Mechi iliyopita dhidi ya Stand United alianza kwa mfumo huu.
Kwa mechi ya ugenini dhidi ya Stand United tena kwenye uwanja ambao eneo la kuchezea ni bovu alikuwa sawa.
Lakini kwenye mechi ya leo ambapo alikuwa nyumbani hakutakiwa kuingia kwa kujihami zaidi.
Abdalah Shaibu “Ninja” na Faisal Salum walikuwa wanakaa karibu na mabeki na kutengeneza watu sita kwenye eneo la kujilinda.
Hii ilikuwa na madhara gani upande wa Yanga?, Yanga ilikuwa na watu wachache kwenye eneo la mbele, kitu ambacho kilikuwa hakiwapi nafasi ya kupata nafasi za wazi nyingi hasa hasa kipindi cha kwanza.
Je, Pamoja na Yanga kuwa na watu 6 katika eneo la kuzuiwa walikuwa imara kwenye ulinzi?
Hapa ndipo ambapo golikipa wa Yanga, Kindoki ninapomlinda. Wengi wanaweza kumrushia lawama kwa baadhi ya magoli.
Lakini makosa yanaanzia kwenye aina ya ulinzi ambao Yanga wanaufanya.
Kwanza mabeki wa pembeni wa Yanga (Paul Godfrey na Gadiel Michael) walikuwa wanakaa juu mwa uwanja kwa muda mrefu.
Kitu ambacho husababisha uwazi eneo lao la nyuma. Kitu ambacho kilikuwa kinampelekea Andrew Vincent kusogea pembeni kuziba uwazi huo.
Alipokuwa anaziba uwazi alikuwa anaacha uwazi eneo la katikati. Na kipindi ambacho alipokuwa anajisahau, basi Yanga ilikuwa inaacha uwazi eneo la pembeni.
Uwazi huu ambao ulikuwa unatengenezwa eneo la nyuma kwa Yanga liliwafanya wapinzani wao wautumie vizuri. Ndiyo magoli yote wamefungwa katika eneo ambalo wapinzani wao walikuwa huru kupiga.
Kwanini Andrew Vincent “Dante” makosa yake huyagharimu timu?
Andrew Vincent “Dante” Mara nyingi huwa anashuka katikati kufuata Mpira , Mara nyingi huwa anakuwa katika eneo ambalo siyo sahihi.
Huwa anapanda sana mpaka katikati. Akipanda huwa anaacha uwazi mkubwa eneo la nyuma. Uwazi ambao unatumiwa vizuri na wapinzani.
Kwa hiyo kabla ya kuanza kumlaumu KIndoki, lazima tuanze kutazama eneo la ulinzi la Yanga. Safu yao ina makosa mengi sana ya kiufundi.