Taifa hili linahitaji Msaada mkubwa sana kwenye Mpira wa Miguu!
Niseme tu sisi kama Sponga tumebeba Dhamana kubwa sana kulikomboa hili Taifa na hatutachoka hata siku moja kuendelea kulipa Msaada Taifa hili Adhimu!
Katika Nchi ya watu wasiojua Boli Mkombozi wao ni Sponga, Sponga limejipambanua kuwa Mkombozi wa Soka sio tu wa Taifa hili bali Afrika Mashariki yote sisi ndio Vinara!
Eeeh! Sponga kuna wauza Ufuta kila siku wanapambana juu na chini kukushusha chini ila wasichojua ni kwamba Sponga wewe ni Dubwana moja kubwa sana sema tatizo Unatokea Kariakoo mtaa wa Msimbenga wakipita Asubuhi wanakuona, Wakipita Mchana wanakuona hata wakipita Usiku wanakuona matokeo yake wanakuona mwenzao tu!
Nakumbuka tulishawahi kutishiwa vitimu vidogo vidogo kutoka mataifa madogo madogo yanayochipukia kwenye Boli! kwa Vipindi kadhaa vya Redio na TV huku Wachambuzi wakimaliza Sifa kuvisifia hivyo vitimu vilivyoibuka Msimu mmoja ama miwili na kuvitaja kama TIMU KALI SANA kwa kuwa tu Havitokei Dar es Salaam! sasa pata picha kama Sponga lingekuwa linatokea Nchi za namna hiyo ingekuwaje kwa Miaka hii Mitano ya kuwaburuza Waarabu tunavyotaka!
Kwa Miaka hii Mitano ya Kulibeba Taifa hili Back to Back kwenye Ramani ya Soka Duniani Wachambuzi wangesemaje? Wachambuzi wangekuwa Wana segment maalum ya Kututishia Timu hilo la Kuitwa SPONGA toka Guinea ya Ikweta huko ama Toka Chad ama Toka Namibia nasema Tungelowa MATE ila sasa Tatizo Sponga tunatokea Kariakoo na Viwanja vya Mazoezi Bunju Complex Arena watasema nini? Watasifia Kipi? Wamejaa Choyo na Chuki!
Chukua hii Sisi kama Sponga tunasema hivi hatutaacha Kutoa Msaada kwenye hili Taifa na Nchi Jirani tutaendelea kuwatoa kimasomaso haijalishi mtajiunga na akina nani miaka yote ili mtuangushe jueni tu kuwa sisi hatutashuka!
Kikubwa tunachowaambia Kadri mnavyojiunga na hao wageni sisi tutaendelea kuwabutua wageni wenu na nyinyi wenyewe hadi pale mtakapotubu! Ndio Msamaha wa Dhambi bado ni TOBA tu haujabadilika!
Wiki hii kulitokea Tukio lisilo la Kawaida pale SA kwa Madiba ambapo Timu ya Kaizer Chiefs na Delegation yao yote walienda kuipokea Ahly na kuwapa Hifadhi kwenye Kijiji chao cha Naturena, Jambo lile likapokelewa kwa shangwe sana hapa Nchini na Kuonekana ni jambo la Kawaida sana sasa Chukua hii!
Kocha wa Mamelodi Sundowns Manqoba Mngqith baada ya Kuichapa Ahly siku ya Jumamosi akihojiwa kwenye Press Conference alisema …..”Wydad Casablanca walikuja kuomba Facilities zetu wajiandae na mechi ya Nusu fainali vs Kaizer Chiefs miezi 6 iliyopita tuliwakatalia kwa kuwa hatukuona Uzalendo kwa Taifa letu kuwasaidia Wapinzani wa Timu inayowakilisha Taifa letu hivyo tukawaambia watafute sehemu nyingine”. Hapa Kulikuwa na Kichaka kwamba Wydad na Mamelodi wangejenga Mahusiano na Bla Bla nyingine nyingi!
Manqoba akaendelea kwa kusema ….”Lakini wao “Chiefs” walienda kuwapokea Ahly wakawapa na Makazi katika kijiji chao cha Naturena na Kila walilolitaka kuelekea kwenye Mchezo dhidi yetu! ila Timu bora imeshinda na Ushindi wetu huu maana yake tumezifunga timu mbili Kaizer Chiefs na Al Ahly!” Hili ni Somo kwetu ametupatia Kocha wa Mamelodi kwamba hizi mambo za kupokea Wageni hata kama Kaizer Chiefs wamefanya sio Sawa kwa Mustakabali wa Mpira wa Nchi na Maendeleo yetu kwa maana Mamelodi wanawakilisha SA!
Sasa hapa kwetu kile kikundi cha Ushangiliaji wajitathmini mwaka wa tano mfululizo huu wanashangilia Wapinzani wetu na TUNAENDELEA KUWABUTUA, Sponga tunasema Msiache na kwa sasa mjitahidi mtengeneze na Facilities muanze kuwapokea huko kwenu ili mjipambanue kama Kaizer Chiefs walivyofanya na sisi TUTAWAPIGA maana Dhima yetu ni Kuusaidia huu Umma wa Watanzania na Afrika Mashariki yote ambayo inajua kabisa sisi ndio Wakombozi wao!
Mwakani tena Timu Nne CAF kwa Msaada wa Sponga nyie Toleweni mapema tu tena Mpigwe Home and Away kama kawaida yenu na sisi tutazilinda Nafasi Nne ambazo tumezileta kwa Kupigana Machozi Jasho na Damu!
Nchi hii bila Sponga ingekuwa UKIWA TENA UTUPU kwenye Ramani ya Boli la Kimataifa!
Ooooh! Sponga Nchi inakulilia Hii endelea kuipa MSAADA, Usichoke maana Hata hadithi za Manabii hakuna aliyewahi kukubalika Kwao!
Sponga endelea kutoa Msaada kwenye hili Taifa!