Mudathir Yahya Abass ni miongoni mwa wachezaji wa muhimu sana kwenye eneo la kiungo la Young Africans tangu msimu uliomalizika chini ya kocha Mohamed Nabi.
Eneo la kiungo la Young Africans linapata ubora wake tangu ajiunge na klabu kuanzia michuano ya ndani mpaka mashindano ya kimataifa! Msimu huu chini ya Miguel Gamondi anaendeleza kile ambacho alikifanya msimu uliopita.
Wakati anaelekea Young Africans aliwakuta Khalid Aucho, Sure Boy, Yanick Bangala na Zawadi Mauya waliokuwa wanacheza kwenye eneo hilo lakini hii haikumpa shida, Mudathir alisubiri nafasi tu ili kuonyesha uwezo wake na kuaminiwa ndani ya timu.
Mudathir amecheza sana na Khalid Aucho kama viungo wawili wa chini wa Young Africans nyuma ya mstari wa juu wa ushambuliaji na wamecheza vizuri sana asilimia kubwa ya mechi ambazo wamecheza kwa pamoja katika eneo hilo.
Kipindi ambacho anajiunga na Young Africans hakuimbwa sana lakini amekuwa mchezaji wa muhimu sana ndani ya uwanja kuna mechi nyingi sana za msimu uliopita hasa za kimataifa alifanya vizuri sana na miguu yake iliamua kwenye baadhi ya matukio ya muhimu mpaka timu ikacheza fainali ya Kombe la Shirikisho la Afrika.
Eneo analocheza kuna ushindani mkubwa sana kwa kuangalia wachezaji waliopo ndani ya timu kwa sasa lakini bado amekuwa akipata dakika nyingi za kucheza na anaonyesha ubora wake kwa kiwango cha juu huku kitu kizuri zaidi Mudathir Yahya ni mchezaji wa ndani.
Nadhani mnakumbuka wakati Feisal Salum ana shida na Wananchii ndio wakati ambao Mudathir Yahya anaingia, kaenda kupewa nafasi na kaitumia vyema! Ule ni wakati ambao wengi walisahau kuhusu Fei Toto sababu mchezaji aliyekuja alicheza vizuri na timu inapata matokeo.
Mudathir Yahya kwa sasa yupo kwenye wakati mzuri sana muhimu ni kuwa na muendelezo wa hichi anachokifanya kwa sasa ndani ya Young Afrikans.
New Zanzibar Financ