Klabu ya Singida utd leo imezungumza na waandishi wa habari na kufafanua mambo mbalimbali yanayohusu klabu kuelekea fainali ya Azamsports FederationCup itayopigwa June 2 Arusha katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Moja ya habari kubwa ni kuweka wazi usajili wao msimu ujao huku ikiwapiga bao Yanga kwa mnyakua winga wa Ndanda aliekua anawaniwa na Wanajangwani!
Usajili uliotangazwa leo na klabu ya Singida utd :
Tiber John kutoka Ndanda fc!
Uongozi wa Singida United umemtangaza mchezaji huyu kuwa mchezaji wake kwa kusaini naye mkataba wa miaka mitatu.
Tiber amejiunga na Singida akitokea Ndanda FC ya Mtwara iliyojikwamua kuepuka kushuka daraja katika mechi ya mwisho msimu uliomalizika.
Mchezaji huyo pia alikua akiwindwa na Yanga.
Amara Diaby ametoka Asec Memosa!