Baada ya leo hii kutajwa orodha ya wachezaji walioachwa na Azam Fc likiwemo jina la Ramadhani Singano “Messi”, kuna habari kuwa mchezaji huyo amejiunga na klabu ya Yanga.
Yanga imekuwa ikijiimarisha kwenye usajili msimu huu baada ya kutofanya vizuri msimu uliopita. Ramadhani Singano ameachana na Azam FC, awali aliwahi kuwa mchezaji wa Simba kabla ya kutimkia kwa matajiri hao wa Chamazi.