Klabu ya soka ya Simba imetangaza kuachana na kiungo wake mshanbuliaji Benard Morrison waliemsajili kutoka Yanga misimu miwili iliyomalizika.
Kupitia taarifa yake rasmi ya klabu Simba imemtakia kila lakheri Morrison huku wakimshukuru kwa mafanikio makubwa waliyoyapata pamoja naye klabuni hapo.
Katika misimu miwili ya Benard Morrison ndani ya Simba walifanikiwa kuchua kombe la FA, Ubingwa wa Ligi Kuu Bara, walifika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika.
Katika taarifa hiyo iliyotolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzales inasema!
Kumekuwepo na tetesi zinazomuhusisha Benard Morrison kurejea klabu yake ya zamani Yanga ambayo aliitumikia kabla ya kujiunga na Simba.
Awali Benard Morrison alikua haonekani na kikosi cha Simba tangu mchezo dhidi ya Yanga ulipomalizika huku sababu mbalimbali zikitajwa ikiwepo majeruhi na matatizo ya kifamilia lakini sasa ni wazi Simba kupitia taarifa hii kwa umma wamefuta utata wote.