Sambaza....

Tulizoea kusikia kwa wenzetu tu na tulizoea kuona kwa wenzetu haswa katika nchi za Kiarabu Afrika Kaskazini na walau bondeni Afrika Kusini jinsi timu zao zinafanya vizuri na kufuzu katika hatua za robo fainali za mashindano makubwa kwa upande wa vilabu Barani Afrika lakini sasa nasisi tumeonja utamu.

Simba na Yanga kwa mara ya kwanza zimefuzu kwa pamoja katika robo fainali ya michuano mikubwa kabisa Barani Afrika. Simba wamefuzu robo fainali wakitokea kundi C la Ligi ya Mabingwa wakati Yanga wao wamefuzu robo fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

 

Na kwa kufuzu huko kumeleta neema ya fedha kwa wababe hao wawili kutoka katika Ligi bora namba tano Afrika. Sasa Simba na Yanga watakwaa mamilioni ya Chama cha Soka Barani Afrika CAF kama ambavyo utaratibu ulivyoweka.

Simba kwa kujihakikishia kufuzu robo fainali wana uhakika wakupata dola 650,00 ambazo ni zaidi ya bilioni moja na nusu kwa pesa za Kitanzania kwa kupenya kwenda robo fainali pekee.

 

Kwa upande wa Yanga wao watapokea kiasi cha dola 350,00 ambazo ni zaidi ya milioni 850,000 za Kitanzania kwa kufuzu kwenda robo fainali. Na kwa Yanga hii ni mara yao ya kwanza.

Neema ya fedha hizo si tu inawakuta Simba na Yanga bali pia Shirikisho la soka nchini TFF wanahusika katika fedha hizo. Ipo hivi kila timu huwa ni lazima ikatwe kiasi cha fedha baada ya kufuzu na kupewa Shirikisho la nchi husika hivyo na wao TFF wana mgao wao kwenye pesa hizo.

Sambaza....