Sambaza....

Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi Simba kimewasili salama kikitokea Algeria walipocheza na JS Saoura na kupoteza kwa mabao mawili kwa sifuri.
Baada ya matokeo hayo Simba haina namna nyingine zaidi ya kuifunga AS Vita siku ya Jumamosi katika uwanja wa Taifa “Kwa Mkapa”, wenyewe wanasema “DO or DIE”

Baada ya kuwasilì tu nahodha John Raphael Bocco ametoa tamko zito kwa mashabiki wa klabu ya Simba kuelekea kwenye mchezo dhidi ya AS Vita.
John Bocco ” Tunamshukuru Mungu tumefika salama, tuna mchezo mwingine dhidi ya AS Vita. Mimi naamini kwa morali tuliyonayo wachezaji pamoja na mbinu za mwalimu (Patrick Aussems) tukiwa nyumbani tutapamabana na Vita na tutafuzu kuelekea robo fainali.”

Simba sc

Nahodha huyo wa Simba alitanabaisha kua wao kama wachezaji wapo tayari kupambana tena wakiwa na morali ya hali ya juu ili kuweza kuandika historia.

Katika michuano ya Klabu Bingwa Africa Simba imekua na historia nzuri katika uwanja wake wa nyumbani ikiutumia kuwaaangusha wapinzani wao waipokutana msimu huu zikiwamo Al-Ahly, Nkana Rangers na Mbabane Swallors.

Sambaza....