Sambaza....

Kazini kwa makipa wa Simba SC kuna kazi. Mstari huu aliwahi kuuandika mlinzi wa Yanga Sc Kibwana Shomary akiuzungumzia umahiri wa mlinzi mwenzake Attohoula Kouassi Yao.

Kazini kwa makipa wa Simba SC kuna kazi kweli. Pengo la kipa wao namba moja Aishi Manula limeonekana waziwazi, licha ya kukosekana kwa miezi saba sasa.

 

Lango la Simba SC haliko salama tangu Manula awe kitandani kujiuguza. Hivi sasa hakuna tofauti kati ya kipa anayeanza, anayekaa benchi hadi wengine wanaokaa majukwaani.

Kinachotokea sasa Manula anayekaribia kurudi kiwanjani ameonekana kutamaniwa zaidi na mashabiki kuliko kawaida.

Aishi Manula.

Makipa walioko sasa wametoa mianya kwa watu kumkumbuka Manula kwa baadhi ya matukio. Kama makipa wake wangekuwa mahili Manula ingemchukua muda
mrefu kurudi katoka nafasi yake.

Kinachotokea sasa. Nafasi ya Manula inaonekana kuwa salama. Akiwa imara tu anarudi katika nafasi yake kiurahisi tu.

Ally Salim.

Kama makipa wale wangekuwa imara ingemchukua muda mrefu Manula kupata nafasi yake. Lakini kinachoitokea Simba SC langoni mwake kumefanya wautamani urejeo wa Manula haraka.

Kuna makipa wamewahi kupata nafasi za kuwa makipa wa kwanza baada ya makipa tegemeo kuumia. Mifano iko mingi.

Ayoub Lakred.

Lakini makipa wote wa Simba SC wameshindwa kuitumia nafasi hii. Sio Hussein Abel, Ally Salim wala Ayoub Lakred wote wametoa sababu za watu kumkumbuka Manula wao.

Sambaza....