Sambaza....

Wapwa: Ulikionaje kiwango chake jana? Binafsi yangu ni moja ya mabeki bora wa kati si nchini tu bali ukanda huu wa East Africa

‘Master of tackling’ ni fundi wa kuingia uvunguni kwa muda muafaka na kwa tendo muafaka ili uweze kufanya tackle kwenye soka, huyu si mwingine ni Henoc Inonga Baka.

Lazima uwe na Concentration + decision + timing iwe katika type zote 3 za tackles ambazo zipo Duniani Block tackle au ‘kibuyu’ Poke , Side tackle jamaa ni ‘mcharo ‘sana

Anticipation ndiyo nyumbani kwakwe Mwamba huyu ana uwezo mkubwa sana kunusa njia za wahalifu kama Mbwa wa Polisi aliyefunzwa vyema akafunzika

Tatizo lake kubwa ninaloliona kutoka kwake ni mipira ya juu Aerial ball ,jamaa hana uwezo mzuri wa kupiga vichwa hasa inapokuja mipira ya kugombea akiwa pekee yake mara nyingi anaweza kureceive kwa kichwa kwa maana ya kuupokea mpira wa juu kisha kuuangushia mguuni na kuanza kuondoka kwa kudribble.

Inapokuja wakati wa kushambuliwa au kushambulia kwa kupitia kichwa hayupo poa sana ,na kwa kuliona hili kwa uwezo wake angekuwa anafunga kwa wapinzani au anafanikiwa kuzuia yeye wasifungwe goli la hivyo.

Jumping force yake si nzuri au kubwa kama ambavyo mabeki wengi hasa wanaocheza professional wanavyoweza kuruka ( dank) angalau futi 2-3 toka chini nadhani eneo hili Onyango ni bora zaidi yake.

Na hii kama utamaduni wa wachezaji wengi watanashati au macheck Bob sitaki kusema (matoz) mara nyingi hawapendi kucheza mipira ya vichwa ,atataka aufanyie timing ‘aunywe’ kwenye kifua ndiyo furaha yake kubwa.

Ukiachilia hilo mwanaume ‘mtu wa mwisho’ wa maana sana kwa kweli.

Tukutane kwenye show ya #10 @tvetanzania
jumatatu – ijumaa saa 6:00-9:00 Alasiri

Sambaza....