Sambaza....

Msemaji wa klabu ya Simba Ahmed Ally amezungumiza tetesi zashambuliaji wao kutoka Zambia Moses Phiri kama ni kelele tu kama ambavyo zipo kelele nyingine.

Ahmed akiongea mbele ya waandishi wa habari alitanabaisha kwamba wanajua kuwa watu wanamtamani mchezaji huyo lakini hawatampata kamwe.

Ahmed Ally alisema “Tetesi za Moses Phiri kuondoka kwenda Yanga SC au timu nyingine niwambie tu wataendelea kumtamani kama wanavyotamani wachezaji wengine,” alisema na kuongeza;

Moses Phiri akifunga bao katika mchezo dhidi ya Ihefu.

“Moses ataondoka Simba siku tukiamua kuachana nae na siku hiyo siioni, hawatampata “General” hata siku moja.”

“Kwanza Moses Phiri anaondokaje Simba. Simba ni sehemu ya wachezaji kutimiza malengo yao, wachezaji wetu ni matajiri, wanaishi maisha ya kifalme.”

Katika upande mwingine pia Ahmed Ally ameuzungumzia mchezo wao wa Jumapili hii dhidi ya Yanga  katika Ligi Kuu na kusema watauza tiketi zote na wataujaza uwanjani huku akisema wanajua umuhimu wa kushinda mchezo huo.

Mara ya mwisho wawili hawa kukutana katika Ngao ya Hisani mkoani Tanga mchezo ulimalizika kwa suluhu kabla ya Simba kushinda kwa matuta.

“Mpira wa Tanzania umejengwa katika Kariakoo Derby ya Simba na Yanga, ni mechi ambayo imebeba kila kitu cha mpira wa nchi hii. Ni mechi yenye thamani kubwa.”

“Mechi ya AFL hatukuuza tiketi zote, walizuia baadhi ya tiketi kwa sababu ya kiusalama, lakini mechi ya KariakooDerby tutauza tiketi zote. Tunataka hadi Ijumaa ikiwezekana tiketi ziwe zimeisha na tunatamani mashabiki wengi tuwe wa Simba,” alimalizia Ahmed

Sambaza....