Sambaza....

Klabu ya soka ya Simba Sc itacheza mchezo wa kirafiki na timu AFC Leopards ya Kenya siku ya Jumamosi ya September 08 katika uwanja wa Taifa Dar majira ya saa 1:00 Usiku.

Mchezo huo ambao unazikutanisha timu zilizo chini ya mdhamini mmoja ambae ni Sportpesa  ni maalum kwaajili ya kuwaweka fiti wachezaji wa timu zote mbili kutokana na ligi kusimama kupisha kalenda ya FIFA.

Kwa upande wa timu zote mbili Ligi zao zimesimama ili kupisha timu za Taifa katika kufuKu Afcon 2019 nchini Cameroon. Timu ya Taifa ya Kenya “Harambee Stars” wao watakua kibaruani dhidi ya Ghana nyumbani huku Tanzania “Taifa Stars” wao watakua na kibarua dhidi ya majirani zao Uganda ugenini.

Viingilio vya mchezo huo vitakuwa 5000 mzunguko, 10,000 VIP B wakati VIP A ni 15,000.

Pia siku hiyo watu ambao watawahi uwanjani watautazama mchezo wa kufuzu AFCON, 2019 kati ya timu ya Taifa ya Uganda dhidi ya Tanzania mchezo ambao utachezwa siku hiyo hiyo ya jumamosi saa 10:00 jioni katika dimba la Nambole Kampala Uganda na itarushwa live na kituo cha Azam TV.

Sambaza....