Sambaza....

Wekundu wa Msimbazi Simba kesho wanashuka dimbani kuvaana na Singida Fountaine Gate Fc katika mchezo wapili wa Ngao ya Hisani.

Simba waliomaliza nafasi ya pili msimu upiopitaitashuka dimbani saa moja usiku kuvaana na washindi wanne wa msimu uliopita Singida FG Fc katika mchezo wenye mambo mazito ndani yake.

Katika mchezo huo Simba Sc itakutana na wachezaji wake walioitumikia timu yao msimu uliopita kwa mara ya kwanza. Benno Kakolanya, Gadiel Michael na Joash Onyango watavaana na muajiri wao wa zamani waliochana hivi karibuni.

Mshindi wa mchezo huo atakwenda kukutana na Yanga katika fainali itayopigwa Jumapili ya Augusti 13 ambae amemfunga mabao mawili kwa sifuri Azam Fc.

Kuelekea mchezo huo kocha wa Simba amesema “Kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho, wachezaji wapo vizuri. Tunafahamu itakuwa mechi ngumu lakini tumejipanga kwa ajili ya ushindi ili tutinge fainali,” alisema na kuongeza;

“Nafurahi kuona wachezaji wapya tuliowasajili wakiingia kikosini na kufanya vizuri. Juzi Willy Onana na Fabrice Ngoma walifunga mabao na wote ni wageni, hilo ni jambo zuri,” amesema Robertinho.

Shomary Kapombe.

Kwa upande wake mlinzi wa kulia, Shomari Kapombe amesema tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Singida lakini tupo tayari kupambana kwa ajili ya timu.

“Ngao ya Jamii ina maana kubwa kuichukua sababu inakupa ramani kuelekea msimu mpya wa ligi utakavyokuwa. Tunajua utakuwa mchezo mgumu lakini tumejipanga kushinda,” alisema Kapombe.

Katika michezo miwili waliyokutana msimu uliopita wawili hao Simba alipata ushindi nyumbani na sare ugenini dhidi ya walima alizeti hao.

Ni wazi mchezo wa kesho utakua ni wa kisasi cha kihistoria kutokana na historia ya timu hizo mbili lakini pia ni mchezo wa mwanzo mpya kwa nyota wa zamani wa Simba

Sambaza....